MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa kulia akiwa na
Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani wakimsubiri Waziri wa Uvuvi na
Mifugo Mh. Luhaga Mpina kufanya nae kikao ikiwa ni mpango mkakati wa
kufanikisha changamoto na utekelezaji wa ubunifu katika sekta ya uvuvi
inayoongoza kwa mapato na kutegemewa na wakazi wengi wa Pangani kulia
ni Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gipson
Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mh. Luhaga Mpina kulia akimlaka Mkuu wa
wilaya ya Pangani Zainabu Issa wakati alipofika ofisini kwake kwa
mazungumzo kufanikisha changamoto na utekelezaji wa ubunifu katika
sekta ya uvuvi
inayoongoza kwa mapato na kutegemewa na wakazi wengi wa Pangani.
Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mh. Luhaga Mpina akiwa na Mkuu wa
wilaya ya Pangani wa pili kutoka kushoto na Katibu Tawala wa wilaya ya
Pangani kulia akiwa na Afisa tawala wa wilaya hiyo Gipson mara baada
ya kufanya mazungumzo nao leo Jijini Dodoma
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Pangani ikiongozwa na Mh. Zainab Abdallah kwa ushirikiano na Ofisi ya Mbunge imefanya ziara ya kikazi makao makuu ya nchi mkoani Dodoma ikiwemo kukutana na kuwa na kikao na Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mh. Luhaga Mpina na kufanikisha changamoto na utekelezaji wa ubunifu katika sekta ya uvuvi inayoongoza kwa mapato na kutegemewa na wakazi wengi wa Pangani.
Akizungumza baada ya kikao hicho Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah alisema kikao hicho kilihusisha agenda nne kubwa muhimu kwa ukombozi wa sekta ya Uvuvi wilayani Pangani ikiwemo Upatikanaji wa mashine ya Storage (Compressor) na Jokofu kwa ajili ya kuhifadhi mazao ya baharini kwa ajili ya soko kubwa la Samaki Pangani Mashariki ambalo ujenzi wake umefanikishwa na mapato ya ndani ya halmashauri.
Hatua hiyo imepelekea Waziri Mpina kuwapongeza kwa jitihada za awali na kuahidi kuwa Wizara yake itatoa fedha ili jokofu na compressor vipatikane mara moja na soko lianze kufanya kazi.
Alisema kuelekea utekelezaji wa kampeni ya “VIJANA NI WAKATI WETU” iliofanyika Wilaya ya Pangani; sekta ya uvuvi ndio iliongoza kwa uandikishaji wa Vijana wengi.
Hivyo pia Mkuu huyo wa wilaya aliwasilisha ombi la kupata Engine za Boti za uvuvi kwa ajili ya vikundi vya vijana walio tayari kujiajiri na kujipatia kipato kupitia sekta hii. Wizara kupitia ruzuku yake itagharamia 40% na 60% igharamie halmashauri husika.
Ambapo kufuatilia ombo hilo Wizara hiyo imeridhia kutoa Engine za kutosha kwa vijana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kupitia Halmashauri itatumia mfuko wa vijana na mfuko wa Jimbo kufanikisha upatikanaji wa Engine hizi ili vijana wapate vifaa hivi vya kisasa na utaratibu utawekwa kupitia Idara ya Vijana ya wilaya juu ya usimamizi na mafunzo. Hii ni ishara ya ukombozi kwa vijana wa Pangani.
Mkuu huyo wilaya alisema pia walizungumzia suala la kuanzishwe kwa Chuo cha mafunzo na utaalamu kwa Sekta ya Uvuvi Pangani ikiwa ni kuelekea kupata muarobaini wa sintofahamu ya Chuo cha KIM kurudi mikononi mwa wananchi na kuwanufaisha zaidi ya ilivyo sasa.
Hatua hiyo ilimlazimu Waziri huyo kuamua kuunda timu ya wataalamu ambayo itakwenda Pangani mara moja kuchunguza suala hili ili ripoti itakayo wasilishwa aweze kuitolea maamuzi kwa maslahi mapana ya wana Pangani.
.
Sambamba na hilo liligusiwa suala la ujenzi wa Soko la Samaki na Dagaa Kipumbwi ambapo Waziri Mpina ameweka wazi kuwa suala hili lipo sasa kwenye mipango ya Wizara na kilichobaki ni Utekelezaji wa haraka. na ikumbukwe mipango ilishawekwa sawa juu ya urasimishaji wa Bandari ya Kipumbwi.
" Sekta ya Mifugo nayo haikuachwa nyuma kwa Waziri kuhahidi upatikanaji wa Rambo la malisho ya mifugo Pangani ikiwa ni faraja iliopotea muda mrefu kwa wafugaji wa Pangani "Alisema.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.