ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 12, 2018

ASILIMIA KUBWA YA WATANZANIA HUPATA UPOFU KUTOKANA NA KUCHELEWA KUPATA TIBA


GSENGOtV


IMETAJWA kuwa asilimia kubwa ya watanzania hupata ulemevu wa macho au pengine upofu wa kudumu kutokana na kuchelewa kupata huduma au kuangukia mikononi mwa wahudumu wa afya wasio na sifa katika tasnia ya udaktari wa macho.

Hayo yamebainishwa hii leo na Rais wa Chama cha Madaktari wa Macho nchini Tanzania Dr. Joseph Masanja wakati wa utoaji huduma bure ya upimaji wa macho uliofanyika katika viwanja vya furahisha jijini Mwanza, huduma ikitolewa na Madaktari wanachama wa Otametria chini ya ufadhili wa Shirika lisilo la Kiserikali la Brien Holden Vision la nchini Marekani.

Amesema kuwa idadi kubwa ya wananchi mijini na vijijini wanapopatwa na changamoto yoyote ya afya ya macho wamekuwa wakikimbilia vituo vya huduma za bei nafuu bila kujali viwango au sifa za wauguzi  wanaowahudumia kwa kuwa inakuwa ngumu kwao kuwabaini.
Rais huyo wa Chama cha Madaktari wa Macho ameiomba Serikali kwa kutumia vyombo vyake vya ulinzi na usalama kuendesha oparesheni kuvibaini vituo vya afya vyenye wauguzi ‘Vishoka’ wanaojiingiza kwenye taaluma ya afya na kutoa huduma za ulaghai zisizo na viwango hali inayosababisha taifa kuwa na idadi kubwa ya watu wenye ulemavu wa macho.

“Vishoka wamekuwa wakiwavutia wateja kwenye vituo vyao kwa kigezo cha unafuu wa bei na hilo ndilo limekuwa tatizo linalosababisha baadhi ya wananchi wenye matatizo hata yaliyo madogo kukomaa na baadaye kuwa makubwa yanayopelekea ulemavu usiotibika, unaotokana na kuchelewa kuzipata huduma sahihi kwa muda na wakati” alisema Dr. Masanja

Kisha akaongeza “ Nawasihi wananchi wanaopata dalili au matatizo au pengine wale wanaotaka kujua afya ya macho, njia sahihi ni kwenda kwenye vituo vya afya vilivyosajiliwa ili wapate tiba iliyo sahihi”

 Mganga Mkuu wa Mkoa Mwanza Dr. Rutachunzibwa Thoma akitoa maelezo kwa wananchi jinsi ya kuzitumia vyema fursa mbalimbali za upimaji afya bure zinazotolewa na taasisi mbalimbali za Serikali na za kiraia. 

Licha ya kuahidi kulifikisha suala la ‘Oparesheni ya kubaini VISHOKA’ mbele ya  kamati ya Ulinzi na usalama inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, Mkuu wa wilaya ya Ilemela Dr. Severine Mlalika aliyekaimu ugeni rasmi  wa Mkuu wa Mkoa kwenye uzinduzi huo, amewataka wananchi kuwa na desturi ya kupima afya za uoni wao mara kwa mara ili kusaidia kujitambua ikiwa ni pamoja na kupata  huduma na ushauri  juu ya namna ya kuishi salama kwani asilimia kubwa ya utendaji na harakati za maisha ya mwanadamu hutegemea macho.

Amesema  kama wananchi watakuwa na mwamko wa kupima afya ya macho, itasaidia  jamii kutambua  na kujiepusha mazingira hatarishi yanavyoweza kuchangia madhara wanayoyapata na namna gani wanavyoweza kuishi salama kwa kujilinda.

Mkuu wa wilaya ya Ilemela Dr. Severine Mlalika akipima afya ya macho kwa moja ya madaktari viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.
Dr. Moes Nasser ambaye ni mmoja wa wafadhili wa huduma hiyo ya upimaji wa macho akitoa ufafanuzi kwa mgeni rasmi  Mkuu wa wilaya ya Ilemela Dr. Severine Mlalika (kulia).
Edden Rodrick ambaye ni Mtaalam wa macho na Mwakilishi mkazi wa Shirika la Brien Holden Vision Institute la nchini Marekani akitoa maelezo kwa Mkuu wa wilaya ya Ilemela Dr. Severine Mlalika jinsi walivyojipanga katika suala la vitendea kazi kwa mpango huo wa upimaji.
Upimaji unaendelea....
Mmoja baada ya mwingine, wakubwa kwa wadogo.
Upimaji ukiendelea.
Kazi ikiendelea.
"Unaiona hii...." ni kama mmoja wa madaktari akimuuliza mwananchi aliyefika hapa kupima afya ya macho yake.


Mkuu wa wilaya ya Ilemela Dr. Severine Mlalika akikata utepe kuashiria uzinduzi wa upimaji afya kushoto ni Dr. Moes Nasser na Mganga Mkuu wa Mkoa Mwanza Dr. Rutachunzibwa Thoma.


Viwanja vya Furahisha.
Mwamko wa wananchi.
 Wananchi wanaozijali afya zao wamejitokeza hapa.
Maelezo mabanda mbalimbali ya utoaji huduma.
Vifaa vya upimaji...
Miwani...
Jicho limeona 'Selfie muhimu'
Huduma zikiendelea nao madaktari wakiendelea kuweka mikakati jinsi ya kufanikisha.
Picha ya pamoja.

ITAENDELEA TAKWIMU ZAJA

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.