ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 2, 2017

WAZIRI MKUU WA UTURUKI AMPONGEZA JPM.

Waziri mkuu  wa Uturuki akisalimiana na watanzania.
WAZIRI  MKUU WA  UTURUKI AMPONGEZA JPM
Edwin  Soko

Istanbul

Uturuki

Waziri  mkuu wa   wa  Uturuki  Binal   Yildirim  amempongeza  Ras  John Pombe  Magufuli na  Watanzania   wote  kwa  kudumisha  ushirikiano wa Nchi hizo mbili  na  kuahidi kuendelea kuulinda  kwa manufaa ya Nchi  zote mbili.


Amezungumza hayo kwenye  ufunguzi  wa kongamano  kubwa la kibiashara  lijulikanalo  kwa   jina  la  Turkish  Exporter’s   Assembly  Week, lililofanyika  kwenye  ukumbi wa  Istnbul  Confress  Center na  kuhudhuriwa na wafanyabishara  zaidi ya  1000  kutoka  Nchi mbalimbali Duniani.


Yildirim  alisema  kuwa,  Rais   Hohn  Pombe  Magufuli ameonyesha  nia  ya    Tanzania na  Uturuki  kufanya kazi ka pamoja    kwa manufaa ya raia  wa Nchi  hizo mbili, hivyo  ni  suala  la   kupongezwa kwani  lina faida  kubwa kwenye  ukuaji wa uchumi   kwa  Nchi  hizo  mbili.


Pia  amewapongeza  watanzania kwa  kuwa  na  historia  nzuri ya  ukarimu na kusisitiza kuwa,   wafanyabisha  wachangamkie  fursa  za kibishara    kwani  Uturuki  ipo  tayari  kufanya   biashara  na Tanzania, kutokana  na  Tanzania kuwa na  bidhaa  nyingi zenye uhitaji  mkubwa  Uturuki, na  pia Uturuki  ina  uwezo wa kiteknonolojia  na  inaweza kusaidia  falsafa  ya uchumi wa  viwanda  kwa Tanzania.


Mfanyabishara  wa Tanzania  Abuu  Kondo , alisema kuwa kongmano  hilo limemsaidia  kupata  wafanyabishara  wapya  wa Uturuki ambao  wengi  wameonyesha  nia  ya  kushirikiana na  watanzania kwenye  Nyanja  mbalimbali  za  kibiashara, hivyo  lina mchango  mkubwa  kwa ukuaji wa  biashara  yake.


Wafanyabishara wa kitanzania walioshiriki kongamano.
Naye Balozi  wa Tanzania  Nchini  Uturuki  Elizebert  Kihondo,  alisema  kuwa,  kongamano hilo  lina  fursa  kubwa  kwa  wafanyabishara  wa kitanzania, kwa kuwa  linawakutanisha   wafanyabishra  wa Nchi  mbalimbali na  wnaweza  kushirikiana  katika  kuhimiza  ujengwaji  wa viwanda Nchini  na kusukuma mbele  ukuaji wa  uchumi wa viwanda.


“Unajua   wenzetu  Uturuki wamekuwa  na  uzoefu sana kwenye  Nyanja  ya viwanda hivyo  basi  tukiwatumia vyema  wanaweza kwenda  nyumbani kama wawekezaji na  kujenga viwanda” alisems balozi  Kihondo.


Naye Makamu wa rais  wa  chama  cha  wafanyabiashara wa viwanda  na  kilimo  Tanzania bwana  Octavian  Mshiu alisema  kuwa,  wafanyabishara  zaidi  ya  ishirini  toka  Tanzania wamepata  nafasi  ya  kuja  kwenye  kongamano hilo ni  matumaini  yake kuwa  watashiriki  kikamlifu  kwenye  kupanua mahusiano na uwekezaji   wa kibishara   kwa kushirikiana  na   wenzao wa  uturuki .


“Sisi kama chama  tutahakikisha  tunazidi kutengeneza  fursa  nyingi  kwa wanachama  wetu za  kupata  nafasi  za kujifunza  uwekezaji   kupitia  mahusiano  tuliyonayo  na  Nchi  ya   Uturuki  pamoja  na  Nchi mbalimbali Duniani” Alisema  Mshiu

Pia wafanyabiashara  wa Tanzania  wao  ndio  pekee  waliopata  naafsi  ya  kuongea  na waziri  mkuu  na  kumkabidhi  zawadi za kiasili  vikiwemo  ninyago    kutoka  Tanzania.


Waziri  mkuu  akihutubia
Historia  inaonyesha   Nchi    ya  Uturuki  na Tanzania zina mahusiano  mazuri  kwenye  Nyanja za kiuchumi    hasa katika  utekelezaji wa miradi  mbalimbali  ya  kimaendeleo  ukiwemo wa  ujenzi wa  reli  ya   kisasa  kutoka  Dar  es Salaam  kwenda  Morogoro.


 Kongamano  hilo    ni la siku  tatu  limenza  Novemba  1  litahitimishwa  Novemba  3 mwaka huu  kwa  wafanyabishara   kukutana  na  wenzao  na  kuwa na majadiliano  yajulikanayo kama  B2 B

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.