Madereva (wenye nguo nyekundu) waliotekwa na waasi wa DRC wakiwa na Gavana wa Bukavu nchini humo. (Na Mpigapicha Maalumu). |
MADEREVA wa malori kutoka nchini Tanzania waliokuwa wametekwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kuokolewa, watawasili nchini leo.
Madereva hao juzi walikutana na Gavana wa Bukavu kuzungumza naye kuhusu maswahibu yaliyowakumba katika tukio hilo la kutekwa lililoripotiwa kutokea Septemba 14, mwaka huu nchini humo kabla ya kuokolewa na majeshi ya Congo (DRC).
Taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyotokewa jana, ilisema madereva hao watawasili nchini leo saa tisa alasiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Rwanda.
Mmoja wa rafiki wa karibu wa mmoja wa madereva wawili waliotoroka, Athuman Fadhili, na raia wa Kongo aliyejitambulisha kwa jina moja la Franco, aliliambia gazeti hili jana kwa simu kutoka Congo kuwa rafiki yake huyo (Fadhili) yupo salama na anajiandaa kurejea nyumbani Tanzania kwa furaha.
“Hana tatizo lolote, yupo salama na sipo naye karibu ungeongea naye, lakini yupo kwa Ubalozi wa Tanzania hapa na wengine wakijiandaa kurejea huko, nadhani mpaka kesho saa tisa mchana watakuwa huko," alisema Franco.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Congo ilieleza kupitia vyombo vya habari vya kimataifa na vya ndani ya nchi hiyo kuwa madereva hao, walikuwa salama baada ya kuokolewa na majeshi ya nchi hiyo kutoka kwa watekaji wenye silaha ambao ni majambazi na si waasi, kama ilivyoelezwa awali. Congo ilieleza kuwa utekaji huo, ulifanyika katika kijiji cha Matete kuelekea Namoya katika mji wa Kivu Kusini mkoani Manyema.
Awali, taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania kwa vyombo vya habari baada ya kutokea tukio hilo, ilieleza kuwa malori 12 yalitekwa katika eneo la Namoya Jimbo la Kivu Kusini katika nchi ya DRC Septemba 14, mwaka huu.
Ilieleza kuwa kati ya malori hayo, manane yanamilikiwa na Kampuni ya Simba Logistics ya mfanyabishara maarufu wa Tanzania, Azim Dewji na mengine ni ya wafanyabiashara kutoka Kenya.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa watekaji ni kikundi cha waasi cha MaiMai na baada ya kuyateka magari hayo, waliwashusha madereva na kuwapeleka porini na kisha kuyateketeza kwa moto magari manane, yote ya Dewji na walitoa saa 24 walipwe fedha Dola za Marekani 4,000 kwa kila dereva ili wawaachie. Madereva wawili walitoroka na kutoa taarifa kuhusu tukio hilo.
Hata hivyo, serikali kwa kushirikiana na Serikali ya DRC, iliwaokoa madereva hao kwa kutumia majeshi ya DRC.

Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.