Mtangazi wa kipindi cha 'Kazi na Ngoma' kupitia Jembe Fm Mansour Jumanne (kulia) akifanya mahojiano na mmoja wa wananchi wa jiji la Mwanza baada ya kujionea hali ya mazingira machafu ya makaburi ya Kitangili. |
Aidha wananchi hao wameziomba mamlaka husika kuweka kanuni na sheria za kuhifadhi na kulinda maeneo ya makaburi hayo ambayo sasa yamegeuka kuwa eneo la uharibifu mkubwa wa kimazigira.
Wakitoa malalamiko yao baadhi ya wakazi wanao fika viwanja hivyo kwaajili ya kuzika ndugu zao wanasema kuwa maeneo hayo ya makaburi yamekuwa yakitoa harufu mbaya baada ya kugeuzwa kuwa dampo la utupaji wa taka , eneo la malishio ya wanyama, kificho cha wezi na waporaji pamoja na akinadada poa wanaofanya biashara ya kuuza miili yao nyakati za usiku.
Wamesema licha ya wananchi kulipa fedha ili kuweza kupata eneo la ardhi kama idhini ya kuzika kila mwili wa ndugu au jamaa wanaofariki dunia lakini bado Halmashauri husika imelifumbia macho suala la kuweka uzio kuzunguka eneo la makaburi ikiwa ni sanjari na kuweka walinzi, suala ambalo sasa linawapa kiburi wananchi kufanya wanavyotaka.
BOFYA PLAY KUSIKILIZA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.