Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula, akitia mkazo kuhusu matumizi sahihi ya vifaa vya usafi alivyo kabidhi na masuala mengine ya utendaji. ZAIDI STORY KAMILI HAPA CHINI. |
Shughuli ya uzinduzi na makabidhiano ya vifaa vya usafi ambavyo ni diaba za kukusanyia uchafu pamoja na fagio kwa machinga wa Makoroboi Jijini Mwanza, imeingia dosari baada Mwenyekiti wa Shirika la Machinga mkoani Mwanza SHIUMA, kutofautiana kauli na Katibu wake, juu ya matumizi ya fedha za mkopo zilizotolewa na halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Hayo yamejili baada kusomwa kwa risala ya machinga katika shghuli hiyo iliyofanyika jana katika eneo la Makoroboi, bila kuainisha kwamba SHIUMA pia ni miongoni mwa vikundi vilivyonufaika na mikopo midogo midogo kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Hali hiyo ilisababisha diwani wa Kata ya Nyamagana na Naibu Meya wa Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha, kuhoji ni kwa nini SHIUMA haikuweka bayana kupokea mkopo wa Shilingi Milioni Moja kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza, hali iliyosababisha machinga kupiga makelele kwa madai kwamba uongozi wa SHIUMA unatumia ndivyo sivyo pesa bila kuwanufaisha wanachama.
Alipotakiwa kutolea ufafanuzi suala hilo, Katibu wa SHIUMA,Venatus Anatory, alikiri uongozi kupokea mkopo wa shilingi Milioni Moja kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kwamba Shilingi Laki Sita kati ya fedha hizo, zilitumika kununua vifaa hivyo vya usafi huku Mwenyekiti wa Shiuma,Matondo Masanja, akisema fedha za mkopo bado zipo na kwamba baadhi ya wanachama watanufaika na fedha hizo kwa njia ya mkopo.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula, ambae alikuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo, amewahimiza viongozi wa Shiuma katika kikao cha utendaji kitakachoketi ijumaa ya wiki hii, kuhakikisha fedha za mkopo zinakopeshwa kwa wanachama na si kufanya manunuzi ya vifaa vya usafi kama Katibu alivyoeleza na kwamba viongozi hao wahakikishe wanakuwa wawazi katika mapato na matumizi ya fedha za wanachama.
CHANZO: BINAGI MEDIA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.