ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 7, 2016

AIRTEL MKWANJIKA YAFANYA MAMBO KWA WAKAZI KANDA YA ZIWA.

Erasmus Mtatuba ambaye ni fundi umeme kutoka mkoa wa Kagera akijizolea fedha toka katika chumba chenye upepo wa kupeperusha fedha ndani ya Droo ya shindano la Airtel Mkwanjiaka ambapo kwa muda wa dakika moja iliyo pangwa alifanikiwa Ku-Kwanjika na kiasi cha shilingi laki saba na kumi. Droo iliyofanyika jana eneo la wazi mbele ya ofisi za Airtel Mwanza.
Erasmus Mtatuba na mkwanja wake ndani ya box la shindano la Airtel Mkwanjiaka.
Tukio lilikuwa linavutia na muda baada ya muda watu hao.....
Ni mwendo wa mahesabu.....
Wadau eneo la tukio.
Kila mmoja anatamani kushiriki mchezo huu.
Mmoja wa washiriki wa Airtel Mkwanjika Erasmus Mtatuba akihojiwa na Jembe Fm live na kusikika katika kipindi cha Drive Mix na hapa alikuwa na mwanadada Natty E.
Sasa ilikuwa ni zamu ya Manyama Makata jamaa anaye jishughulisha na uvuvi wilayani Sengerema mkoani Mwanza kutinga ndani ya Box la upepo na Kukwanjika na Airtel ambapo alifanikiwa kudaka mkwanja kiasi cha shilingi laki sita na themanini.
Wadau nao wanatamani kushiriki Airtel Mkwanjiaka.
Mara baada ya dakika moja ya Manyama Makata kumalizika, Mc Lulu alimfungulia mlango toka wa Box la upepo la Kukwanjika na Airtel ambapo alifanikiwa kudaka mkwanja kiasi cha shilingi laki sita na themanini kwaajili ya mahesabu.
Mahesabu yakifanyika.
Sasa ilikuwa ni zamu ya Eunice Thomas  mkazi wa Buzuruga mjasiliamali kutinga ndani ya Box la upepo na Kukwanjika na Airtel ambapo yeye alifanikiwa kudaka mkwanja kiasi cha shilingi laki saba na sitini elfu.
"Ayaa mimi waombee nisiingiemo, ntazisombaje? wananchi walisikia wakisemezana.
Eunice Thomas  mkazi wa Buzuruga mjasiliamali kutinga ndani ya Box la upepo na Kukwanjika na Airtel akihesabu mkwanja wake alifanikiwa kudaka kiasi cha shilingi laki saba na sitini elfu.
Ni zamu ya Filbert Nyomi toka Kagera kukwanjika.
Wadau wakifurahia umahiri wa Filbert katika kudaka mkwanja wa Airtel Mkwanjika.
Filbert Nyimi ambaye ni mfanyabiashara toka mkoani Kagera alifanikiwa kudaka shilingi laki nane na hamsini.
Safiiii.
Eh bana eh.
Nyingine zilijinasa zenyewe kwenye harakati....
Ikawa zamu ya Eugine Tryeson ambaye ni mkulima toka mkoa wa Kigoma ambapo alifanikiwa kudaka mkwanja wa shilingi laki sita na arobaini. 
Mc lulu wa Sahara Media akifurahia jambo mara baada ya kumaliza kazi jukumu la siku ya kwanza kwa wakazi wa Kanda ya ziwa kukwanjika na Airtel...Zoezi bado linaendelea.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.