NA PETER FABIAN, MAGU.
KAYA zaidi ya elfu 20 za wananchi wanaoishi katika Vijiji, Mitaa na Kata za Mikoa ya Kanda ya Ziwa wamelengwa kufungiwa mitambo ya umeme wa nishati ya jua (Sola) kwa gharama nafuu kutokana na kuwa pembezoni na kutofikiwa na umeme wa gridi ya Taifa wa Shirika la Umeme Tanesco hapa nchini.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi Mwenyeji na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri, Kampuni ya Mobisol Uk Ltd ya jijini Arusha, Livinus Manyanga, katika hafla ya uzinduzi rasmi wa ofisi za tawi lake eneo la Kanyama Kata ya Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza.
Manyanga kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufanya uzinduzi huo, alisema kuwa Kampuni ya Mobisol Uk Ltd ni ya nchini Ujerumani ilianza shughuli zake hapa nchini mkoani Arusha mwaka 2011na kujitanua zaidi katika Ukanda wa Mikoa ya Kaskazini ya Manyara, Kilmanjaro na Arusha na sasa imeingia Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
“ Lengo ni kupunguza umasikini wa upatikanaji wa nishati ya umeme hapa nchini kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya nishati vijijini , kuangaza maisha ya jamii zetu na kufanya mazingira kuwa sehemu bora ya kuishi kutokana na kufungiwa mitambo ya Sola za majumbani ambazo ni endelevu na rafiki kwa mazingira,”alisema.
Mobisol. |
Wadau wa Mobisol |
Mitambo ya Sola Energy ya Mobisol imekidhi vigezo vya ubora wa kimataifa na huuzwa kwa bei nafuu na kwa mkopo wenye liba ndogo kwa wateja wake wanaofika katika ofisi za tawi la Kampuni, pia ombi letu ni ushirikiano na wananchi na Serikali ya Mkoa wa Mwanza kutupatia eneo la wazi kuweza kutoa elimu ya mitambo yetu ili kuwashawishi wateja kabla ya kuwafungia.
Ujumbe madhubuti ulipenyezwa kupitia maigizo. |
Naye mgeni rasmi mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, Mhandisi wa Maji na Umwagiliaji kutoka Sekretalieti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Aron Kolongwa, alipongea ujio wa Kampuni hiyo mkoani humo na Kanda ya Ziwa na kuishukuru kwa kutoa mitambo mitano ya Sola ambapo itafungwa katika maeneo ya shughuli za utoaji huduma za kijamii.
Kolongwa alisema kuwa kupatikana kwa wadau wa maendeleo wa nishati ya mumeme wa sola kutaongea kasi ya maendeleo katika maeneo ambayo hayajafikiwa na nishati ya umeme wa gridi ya taifa na kusaidia wananchi kujikwamua na umasikini kwa kutumia umeme wa sola katika mwanga na biashara na kuimalisha ulinzi katika maeneo ya makazi yao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.