ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 4, 2014

TUZO YA OSCAR YATINGA KENYA.

Kama ilivyokuwa imetarajiwa na wengi mwigizaji mashuhuri kutoka Kenya Lupita Nyong'o amenyakuwa tuzo la Oscar la mwigizaji msaidizi wa kike kwa jukumu lake la kuelezea masaibu ya Patseh katika filamu ya utumwa ya ''12 Years A Slave.''
Baada ya kupokea tuzo hilo Lupita amesema " Haikwepi mawazo yangu kwamba hata dakika moja ya furaha katika maisha yangu ni shukran na maumivu makubwa kwa mtu mwingine.''

Mwigizaji Jared Leto alinyakuwa tuzo la mwigizaji bora msaidizi wa kiume kwa jukumu lake la kuelezea maisha ya mwanamke aliye na jinsia mbili aliyekuwa na akiishi na virusi vya HIV katika filamu Dallas Buyers Club.Kisha Lupita akaongeza kusema, " Na iwe ukumbusho kwangu na kila mtoto kwamba kokote unakotoka, ndoto zako ni halisi.''
Alilazimika kupunguza uzani kwa kipindi kifupi ili kuigiza.
Sherehe ya kutolewa kwa tuzo hizo zimefanyika mjini Los Angeles nchini Marekani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.