ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 4, 2014

TFF WAWAFUNDA VIJANA ILI KUWA WANASOKA WA KIMATAIFA MASHINDANO YA ALLIANCE 2014 YALIYO FUNGULIWA JANA JIJINI MWANZA.

Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Vijana na mjumbe wa Kamati ya Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Bw. Ayuob Nyenzi akipiga penati kufungua  rasmi Mashindano ya Alliance Schools Tournament, uliofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Awali kabla ya ufunguzi wa Mashindano ya Alliance Schools Tournament washiriki walifanya maandamano yaliishia katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Washiriki wa Mashindano ya Alliance Schools Tournament wakiwa kwenye paredi uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kushuhudia uzinduzi.
Kikitumia zana za asili za burudani hiki ni kikosi cha uhamasichaji na ushangiliaji cha Alliance kikichagiza Mashindano ya Alliance Schools Tournament kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Sehemu wa washiriki wa Mashindano ya Alliance Schools Tournament kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Arusha.
Alliance Mwanza.
Benchi la Arusha.
Nao waamuzi ni vijana wanaochukuwa kozi za uamuzi wa soka katika kituo cha Alliance Academy jijini Mwanza. 
Katika mchezo huo wa ufunguzi uliochezwa majira ya saa 8:00 mchana uliozikutanisha timu za vijana (umri miaka 17) za Alliance Academy (Jijini Mwanza) na Future (Jijini Arusha) ilishuhudia Alliance  ikiibuka na ushindi wa gori  2-1 yaliyofungwa na mchezaji Martin Kigi na lile la Future likipachikwa mapema kabisa na Suleiman Yunus.
TFF YAWAFUNDA VIJANA ILI KUWA WANASOKA WA KIMATAIFA MASHINDANO YA ALLIANCE 2014.
Na PETER FABIAN
MWENYEKITI wa Kamati ya Soka la Vijana na mjumbe wa Kamati ya Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Bw. Ayuob Nyenzi jana alifungua rasmi Mashindano ya Alliance Schools Tonament kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Mashindano hayo yanayoandaliwa na Shule ya Alliance Sport s Academy kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, 15 na 13 kwa mwaka wa pili mfululizo na kufanyika Jijini hapa yanashirikisha timu za vijana wa umuri huo za wavulana na wasichana kutoka Mikoa nane kati ya 12 iliyokua umethibitisha kushiriki kutoka awali mwaka huu.

Akizungumza katika ufunguzi wa mashindano hayo Bw. Nyenzi alisema kuwa amefungua mashindano hayo akiteuliwa kumwakilisha Rais wa TFF Bw. Jamal Malinzi ambaye alikuwa awe mgeni rasmi hivyo kwaniaba ya TFF ambayo itaendelea kushirikiana na Walimu na shule zinazoendeleza vyema soka kutoa sekta mbalimbali ikiwemo Aliiance  katika mpira wa miguu hapa nchini.

“TFF inapongeza juhudi kubwa za kuendeleza soka la vijana na kuandaliwa kwa mashindano haya kwa mwaka wa pili mfululizo chini ya Kituo cha Shule za Alliance Schools Sport Academy zilizo chini ya Kampuni ya Nyamwaga ya Jijini Mwanza”alisema

Mjumbe huyo wa TFF alisema kwamba, Shirikisho la mpira wa miguu nchini litaendelea kusaidia katika kuandaa mashindano mbalimbali ya mpira wa miguu kwa kushirikiana na Kituo cha Alliance na sehemu mbalimbali ya nchi hii kwa lengo la kukuza vipaji na kuviendeleza.

“Hakuna nchi yoyote hapa duniani inaweza kupata maendeleo ya soka bila kuwa na msingi wa awali ambazo ni shule za soka la vijana, kwa kutambua hilo TFF imechukua jukumu kubwa la kumtuma kuja Jijini Mwanza kumuwakilisha Rais Bw. kuja kufungua mashindano haya kwa kutambua kuwa vijana ndiyo nguzo la soka la badae” alisisitiza.

Wito wa  kwa vijana ni lazima mtambue malengo yenu mnayoyatarajia siku za mbeleni katika kuendeleza vipaji vyenu, ili uendeleze kipaji chako ni lazima uzingatie nidhamu, kujituza na kufuata maadili ya mpira kwa sasa mko hatua za mwanzo tu kufikia malengo mliyonayo kwani walimu wenu wanalo jukumu la kuwafundisha na nyinyi sasa ni jukumu lenu kuzingatia.

“Epukeni kujiingiza kwenye vitendo vibovu na vilivyo nje ya maadili kwani mpira siku zote una maadili pia hakuna mpira wa miguu utakaoujua kijana na ukawa mchezaji wa juu bila kufuata maadili eti kwa sababu ya kujiingiza katika tabia zisizofaa na za hovyo hovyo hivyo TFF itakuwa karibu na sekta hizi za kuendeleza vijana katika soka kwa kukemea tabia mbaya kwa vijana.

Aliongeza kuwa vitendo itakavyokemea ni uvutaji bangi, kujiingiza katika mapenzi katika umri mdogo,kutokana na vijana wengi kujiona wanaweza kucheza mpira na kuanza kujiingiza katika mapenzi, uvutaji bagi na kuwa walevi wa pombe ambavyo si vitendo vya kimchezo jambo ambalo litauwa vipaji vya soka kwa vijana.

Aidha mashindano hayo yanashirikisha timu za mikoa nane kati ya 12 kutoka Mikoa ya Mwanza, Arusha, Kigoma, Mara, Dar es salaam, Singida , Tabora  na Geita ambapo timu za vijana kutoka shule zenye vituo vya Academy zinazoendeleza vijana kisoka.

Katika mchezo wa ufunguzi uliochezwa majira ya saa 8:00 mchana uliozikutanisha timu za vijana (umri miaka 17) za Alliance Academy (Jijini Mwanza) na Future (Jijini Arusha) ilishuhudia Alliance  ikiibuka na ushindi wa gori  2-1 yaliyofungwa na mchezaji Martin Kigi na lile la Future likipachikwa mapema kabisa na Suleiman Yunus.


Mchezo wa pili uliochezwa majira ya saa 9:15 ulizikutanisha timu za vijana (umri wa 17) za Bom bom (Jijini Dar es salaam) na Mara na matokeo Bom bom iliifunga Mara bao 1-0 na leo mashindano hayo yaliyo katika makundi matatu ya miaka 17, 15 na 13 yanaendelea katika uwanja wa CCM Kirumba, Alliance Girls na Boys Katani Mahina na Uwanja wa  Nyamagana.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.