ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, January 15, 2014

KAULI YA MSINDAI KUSEMA 'WENYEVITI WA CCM TZ BARA WAKO NYUMA YA LOWASSA' YAPINGWA NA WANACHAMA WA UMOJA HUO.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Joseph Msukuma akizungumza na waandishi wa habari hii leo katika ukumbi wa CCM mkoa wa Mwanza. 

WENYEVITI wa CCM mikoa ya Tanzania bara wametoa tamko la kumkana Mwenyekiti wa Umoja wa Wenyeviti CCM Taifa Mgana Msindai, na kutishia kumvua madaraka ya Uenyekiti wa Umoja huo, kwa kuwauza wenyeviti wenzake kwa  watu wanaotarajia kugombea urais kabla ya muda na utaratibu wa Chama kufika.

Hatua hiyo inafuatia tamko lililotolewa kwa niaba ya Wenyeviti wa CCM wa mikoa ya Tanzania bara Joseph Msukuma (Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita) leo jijini Mwanza akipinga kauli iliyotolewa hivi karibuni na Msindai ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, wakati alipoalikwa katika sherehe ya kuuaga na kuukaribisha mwaka mpya wilayani Monduli, hafla iliyoandaliwa na Mjumbe wa NEC na mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa ambapo Msindai katika salamu zake alinukuliwa na vyombo vya habari na taarifa zake kutoka leo akisema kuwa yeye pamoja na wenyeviti wa CCM wa mikoa yote nchini wako nyuma ya Lowassa wakimuunga mkono, kauli ambayo imewaweka katika wakati mgumu wenyeviti wa CCM mikoa mbalimbali hapa nchini ikihofiwa kuanza kuwagawa wananchi na kutengeneza makundi. (BOFYA PLAY KUSIKILIZA TAMKO)

Sehemu ya wanahabari, kutoka kulia ni John Maduhu (Mtanzania), Mashaka Bartazar (Majira) na Deus Bugahilwa.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Joseph Msukuma akizungumza na waandishi wa habari hii leo katika ukumbi wa CCM mkoa wa Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.