ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, January 15, 2014

RAIS WA TFF KESHO KUSAINI MRADI WA UBORESHAJI UWANJA WA NYAMAGANA MWANZA.

Rais wa TFF Jamal Malinzi akijibu maswali yawandishi wa habari jijini Mwanza kwa masula mbalimbali kama sehemu ya maboresho na ukuzaji vipaji vya soka kwa maslahi ya taifa. Nikatika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza ambapo pia rais huyo alishuhudia mchezo wa ufunguzi wa ligi soka daraja la nne baina ya Chipukizi na Alliance Academy uliomalizika kwa Alliance kuibuka na ushindi wa bao 2-1.
Ziara ya kwanza ya Rais mpya wa TFF nje ya makao makuu yake yaliyopo jijini Dar es salaam imeanza leo ambapo rais huyo ametua jijini Mwanza kushuhudia ukuzaji wa soka mkoa wa Mwanza sanjari na kutembelea pia kukagua kituo cha elimu na kukuza michezo cha Alliance Sports Academy kwaajili ya maandalizi ya soka la baadaye nchini
Ni salaam mchezo wa ufunguzi wa ligi soka daraja la nne baina ya Chipukizi na Alliance Academy uliomalizika kwa Alliance kuibuka na ushindi wa bao 2-1.

Patashika dimbani mchezo wa ufunguzi wa ligi soka daraja la nne baina ya Chipukizi (blue) na Alliance Academy (yelow) uliomalizika kwa Alliance kuibuka na ushindi wa bao 2-1.


Wakifuatilia mchezo ndani ya uwanja wa Nyamagana, Kutoka kushoto ni Rais wa TFF Jamal Malinzi, Mwenyekiti wa MZFA Jackson Songora, Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula na Katibu wa Chama cha soka mkoa wa Mwanza (MZFA) Nasib Mabrouk.
Kwa umakini toka jukwaani ni wadau wa soka mkoa wa Mwanza wakifuatilia mchezo wa ufunguzi wa ligi soka daraja la nne baina ya Chipukizi na Alliance Academy uliomalizika kwa Alliance kuibuka na ushindi wa bao 2-1.
Laiti kama uwanja huu ungekuwa katika hali ya ubora zaidi hususani eneo la kati dimbani, tungeshuhudia soka lenye mvuto wa aina yake kwa kulikuwa na ufundi wa hapa na pale ulioonyeshwa na vijana wa pande zote mbili.



Wadu wa soka na kona yao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.