Wabunifu mitindo Jackline Kibacha na Anna Lukindo wakisindikizwa na Mama Balozi Joyce Kallanghe na Mama Rose Kiondo |
Nje ya Jumba la Somerset . |
Wanamitindo wa Kitanzania kwenye London Fashion Week 2013. Anna Lukindo, Christine Mhando, Jacquline Kibacha |
Mama Rose Kiondo, Samson Soboye, Mama Joyce Kallaghe, Anna Lukindo, Christine Mhando, Jacquline Kibacha |
Anna Luks |
Anna, Jack na Duane kutoka Jamaica |
Barabara ya The Strand copy |
London Fashion Week 2013 |
-Imeandikwa
na Urban Pulse na Freddy Macha
-Picha zote za Urban Pulse
Jumapili mchana wilaya
ya Westminster jijini London ilikuwa na mashindano ya
ubunifu na urembo katika maonyesho ya kimataifa ya London Fashion Week. Mashindano haya yalifanyika jumba la Somerset lililosimama imara kwenye
upembe wa kaskazi
ya mto Thames.
Maonyesho ya London
Fashion Week, bado yanaendelea jumba hili la Somerset toka tarehe 14 hadi
tarehe 28. Wiki hizi mbili nzima zitakutanisha kila mtu anaye husika na
biashara ya mavazi na urembo. Magwiji na mapapa wa mitindo, wabunifu,
walimbwende, watafuta vipaji, wafanya biashara, wazalishaji mali ghafi na
wamiliki viwanda. Wote hukutana katika maonyesho
haya. Hapa si vipaji tu vinavyojionyesha, bali pia watu wa biashara.
Siku hii Tanzania
ilikuwa moja ya nchi mbili tu za Kiafrika zilizochaguliwa na British Council na
LFW kushiriki kwenye mashindano ya kutafuta vipaji chipukizi kwenye
tasnia ya ubunifu wa mavazi na urembo. Watanzania Anna Lukindo,
Jacqueline Kibacha na Christine Mhando ndio wasanii
waliobeba bendera ya taifa letu na kutuwakilisha katika mashindano haya ya
kimataifa yanayofanyika kila mwaka kwa zaidi ya miaka 27 sasa.
Katika kuunga mkono
maendeleo ya Tanzania na Watanzania, Ubalozi wetu Uingereza na Bodi ya Utalii
Tanzania, nao pia walichukua nafasi hii kuwasaidia wananchi hawa kufanikisha
mahitaji yao ya ushindani. Ubalozi umetoa Ukumbi wa Nyumba Ya Tanzania ulioko
Bond Street ili wasanii hao waweze kuonyesha nguo na sanaa zao kwa juma zima
kama sheria za London Fashion Week zinavyoamuru. Vile vile Bodi ya Utalii ya
Tanzania imesaidia katika mchango wa mali ghafi zilizotumika
katika shughuli hizi ili kuiuza Tanzania kimataifa.
Mshindi wa tukio alikua
Estonia. Ingawa Tanzania
haikuwa mshindi wa mwanzo- ilichaguliwa kati ya Kumi Bora jambo ambalo
limetikisa nyoyo na vichwa vya waandaaji, wabunifu,wafanya
biashara na watafuta vipaji vya kimataifa. Hii ni mara ya kwanza kwa taifa letu
kushiriki katika shughuli na wote wameguswa na kupumbazwa na usanii
wa hali ya juu ulioonyeshwa na wasanii watatu wa Kitanzania. Lukindo, Mhando na Kibacha wamechukua nafasi
waliyopewa kwa mikono miwili na wote wameisogeza Tanzania hatua moja zaidi
ndani ya ulingo wa kimataifa na katika biashara hii ya mavazi na urembo ambayo
inasemekana ina thamani ya Pauni Billioni 10 ama shilingi
Trillion 25 za Tanzania.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.