ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, February 21, 2012

MH. JOSEPH MBILINYI 'SUGU' NA RUGE MUTAHABA WAMALIZA TOFAUTI ZAO

Kutoka kushoto ni Nchimbi, Sugu, Ruge na Lisu.
Hatimaye Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo Emmanuel Nchimbi amesuluhisha ugomvi uliokuwepo baina ya Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Mkurugenzi wa Clouds Media Lugemalila Mutahaba.

Nchimbi amemaliza ugomvi huo ambao umedumu kwa takribani miaka mitatu baana ya kufanya vikao kadhaa na wawili hao na hatimaye kusaini mkataba wa kumaliza tofauti zao zilizokuwepo hao kabla..Akizungumza na wandishi wa habari hii leo Nchimbi amesema ugomvi mkubwa uliokuwa unawahusu wawili hao ni kuhusiana na masuala ya maslahi na haki za wasanii ambapo sasa wameamua kuachana nao na kuendelea na shughuli zao.

Amesema miongoni mwa mambo waliyokubaliana ni kumaliza mgogoro n uhasama baina yao, wanashirikiana kufanikisha haki na jitihada ya kuinua maslahi ya wasanii, kufanya jitihada ya pamoja ya kuunganisha vyama vya wasaniivya TUMA na TFU ili kutetea maslahi ya wasanii wakiwa na umoja zaidi.

Nchimbi amesema suala la mwisho ambalo wawili hao pia wamekubaliana ni watu wote wanaowaunga mkono katika mgogoro waliokuwa nao wamalize uhasama na kufungua ukurasa mpya na ushirikiano baina yao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.