ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, March 9, 2025

MAMA KOKA AUNGANA NA WANAWAKE WA SF GROUP KUTOA MSAADA KWA VITUO VYA WATOTO YATIMA KIBAHA MJI

 

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA


Wafanyakazi wanawake wa kampuni ya Sf Group ya Jijiji Dar es Salaam wameungana kwa pamoja na baadhi ya wanawake  wa CCM katika jimbo  la Kibaha mji na kutoa msaada wa mahitaji mbali mbali katika kituo cha afya Mkoani pamoja na vituo vya watoto yatima na wenye mahitaji maalumu.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wenzake Mkurugenzi wa rasilimali watu  na utawala wa kampuni ya Sf Group Maria Faustine  amebainisha kwamba wameaamua kutumia maadhimisho ya sherehe za siku ya mwanamke duniani kutembelea maeneo mbali mbali na kutoa msaada kwa wa mahitaji mbali mbali kwa ajili ya kuweza kuwasaidia watu na makundi yenye wahitaji.


Mkurugenzi huyo amebainisha kwamba wameweza kuchangia na kutoa msaada wa vitu mbali mbali vikiwemo sukari, sabuni, mchele, mafuta ya kula  , unga, miswaki, dawa ya meno pamoja na mahitaji mengine  muhimu ambapo jumla ya vitu vyote vimegharimu kiasi cha shilingi zaidi ya milioni 4 .

"Tumeshiriki kikamilifu katka siku ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani na sisi kama wafanyakazi wanawake wa kampuni ya Sf, Group tumeweza kufanya matendo ya huruma na kutembelea katika vituo vya kulelea watoto yatima pamoja na wale wanaoishi katika mazingira magumu na tumetembelea  kituo cha afya mkoani na tumetoa msaada wa mahitaji mbali mbali,"alisema Goreth.

Kwa upande wake Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mama Selina Koka amebainisha kwamba wameamua kuungana kwa pamoja kati  ya waafaanyakazi wa Sf Group pamoja na  baaadhi ya wanawake wa wa CCM katika kwenda kuwatembelea watu mbali mbali wenye mahitaji.  

Naye Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe.Silvesty Koka amesema kwamba lengo lake kubwa ni kuendelea kuwasaidia watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu na kwamba ataendelea kushirikiana bega kwa bega na wamiliki wa vituo hivyo katika kuendelea kuwasaidia katika mambo mbali mbali.
Naye Diwani wa kata ya Pangani Agustino Mdachi amewashukuru wanawake hao kutoka kampuni ya SF Group pamoja na Mke wa Mbunge kwa kuweza kwenda kutoa msaada katika vituo vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Nao baadhi ya wanawake waliojifungua waliopata fursa ya kutembelewa katika kituo cha afya mkoani na wamemshukuru kwa dhati Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mama Koka pamoja nawanawake wa Kampuni ya Sf Group kwa kuweza kuwapatia mahitaji na msaada wa vitu mbali mbali.

Wafanyakazi wa SF Group wameweza kutumiamia maadhimisho ya siku ya mwanamke Duniani ambapo imeweza kutembelea kituo cha afya Mkoani  na kutoa  msaada  katika wodi ya wananawake ikiwa sambamba na kutoa msaada  katika vituo vya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu katika kata za Misigugusugu pamoja na kata ya Pangani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.