ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, March 9, 2025

MIAKA MINNE YA SAMIA WANAHABARI MWANZA WAJA NA MAFIGA MANNE

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Wanahabari mkoa wa Mwanza wameandaa kongamano la "Mafiga Manne' litakalofanyika Machi 18 mwaka huu, likilenga kutathmini maendeleo yaliyofanyika ndani ya miaka minne ya utawala wa Rais Samia Suluhu. Linatarajia kuhudhuriwa na washiriki kati ya 3,000 hadi 3,500 yakiwemo makundi mbalimbali kama wakulima, wavuvi, waendeshaji wa vyombo vya usafiri wa umma, ikiwemo pikipiki (bodaboda) na wafanyabiasha wasodo,alisema Mratibu wa Kongamano, Aloyce Nyanda, jana. "Tukumbuke kwamba Rais Samia aliingia madarakani Machi 19, sisi tunafanya kongamano siku moja kabla ambapo washiriki watapewa nafasi ya kuuliza maswali na kutoa maoni kuhusu maendeleo aliyofanya, ni wapi pamekamilika na wapi bado kuna pengo," alisema na kufafanua zaidi kwamba: Mwaka jana lilifanyika kongamano kama hilo kwa jina la 'Mafiga Matatu', ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akaulizwa maswali na kuyajibu akielezea hali ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na hatua uliyofikiwa. Kwa mfano, alisema Nyanda, Waziri Mkuu aliulizwa kuhusu umeme wa uhakika utapatikana lini, akawahaidi watanzania kwamba changamoto hiyo itatatuliwa muda mfupi. "Na kwa tathmini tuliyofanya sisi waandaaji wa Kongamano tumegundua ahadi ya Waziri Mkuu imetimia, nishati hiyo sasa ni ya uhakika, hasa baada ya bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere kuanza kufanya kazi," alisema. #samiasuluhuhassan

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.