ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 19, 2024

DUBE APIGA HAT TRICK YANGA IKISHINDA 3-2 DHIDI YA MASHUJAA.

 


MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam.

Nyota imemng’aria mshambuliaji wa Kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube Mpumelelo aliyefunga mabao yote matatu dakika za saba, 21 na 53, wakati mabao ya Mashujaa yamefungwa na David Ulomi dakika ya 45 na Idrisa Stambuli dakika ya 62.

Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 30 na kurejea nafasi ya tatu, ikizidiwa pointi moja na watani, Simba SC baada ya wote kucheza mechi 12 na wote wapo nyuma ya Azam FC yenye pointi 33 za mechi 15.

Kwa upande wao Mashujaa baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 19 za mechi 15 sasa wakibaki nafasi ya saba.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.