ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 19, 2024

JESHI LA ZIMAMOTO PWANI LATOA ELIMU KWA WANANCHI 600 KUPAMBANA NA MAJANGA YA MOTO

 NA VICTOR MASANGU, PWANI

 
Jeshi la  zimamoto ya uokoaji Mkoa wa Pwani katika kuhakikisha inapambana  na kuzuia  majanga ya moto imeamua kuendesha zoezi la kutoa elimu na mbinu  kwa vitendo katika makundi  mbali mbali ikiwemo wakinamama wajasiriamali kwa lengo la kufahamu jinsi ya namna kukabiliana na  moto  pindi unapotokea.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Pwani  Mrakibu mwandamizi Jenifa Shirima wakati wa maonesho ya nne ya viwanda,biashara na uwekezaji amebainisha kwamba kwa kipindi cha siku nne  wameweza kufanikiwa kuwafikia zaidi ya wananchi 600 ambao wamenufaika na elimu mbali mbali inayohusiana na masuala ya kupambana na kuzima moto.

Kamanda huyo amebainisha kwamba lengo kubwa la kutoa elimu hiyo kwa ajili ya kuweza kujifunza namna ya kupambana na majanga la moto  katika maeneo mbali mbali ikiwemo katika maeneo ya makazi ya watu wanayoishi , mashuleni, sambamba na maeneo mengine yenye mkusanyiko wa watu wengi.

"Sisi kama jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Pwani tumeamua kushiriki katika maonesho haya ya viwanda, biashara na uwekezaji na tumetumia fursa hii katika kutoa elimu na mbinu mbali mbali kwa wananchi wetu na tumefanikiwa kuwafikia wananchi zaidi ya 600 kutoka katika makundi mbali mbali wakiwemo mama lishe, wakinababa, vijana, viongozi, wafanyakazi wa hotelini, pamoja na wanafunzi kutoka shule mbali mbali,"alisema Kamanda Jenifa.

Kamanda aliongeza kwamba kwa sasa wameweka mikakati ya programu endelevu ambayo itakuwa ikiendelea katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Pwani katika kutoa hamasa kwa wananchi ya kuweza kutumia nishati  safi na salama ikiwa sambamba kutoa elimu juu ya kupambana na majanga ya moto.

Katika hatua nyingine Kamanda huyo amempomgeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha matumizi mazuri ya nishati safi na salama na kwamba na wao wataendelea kumuunga mkono katika kuwaelimisha zaidi wananchi umuhimu wa kutumia nishati safi.

"Wananchi  wa Mkoa wa Pwani ninawaomba pindi majanga ya moto yanapojitokeza wanatakiwa kutoa taaarifa mapema kwa mamalaka ambazo zinahusika na wanatakiwa wapige simu namba 114 kwa ajili ya kupata huduma ya haraka kutoka kwa wahusika ili waje kwa aajili ya kuudhibiti moto,"alisema Kamanda.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha habari na elimu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Pwani Joyce Kapinga amewahimiza wananchi wa wote wa Mkoa wa Pwani kuhakikisha wanazingatia maelekezo yote ambayo wanapatiwa kutoka kwa wataalamu ikiwemo kuwakumbusha kufunga milango yote na madirisha pindi janga la moto linapotokea majumbani mwao.

Nao baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Pwani ambao wamepata fursa ya kupatiwa elimu ya kupambana na majanga ya  moto wamelipongeza jeshi la zimamoto na uokoaji kwa kuweza kuona umuhimu mkubwa kwa kutumia maonesho hayo kwa kutoa elimu na mbinu ambazo zitaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa pindi moto unapotokea.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.