NA ALBERT GSENGO/MWANZA.
Kupitia tafiti mbalimbali zilizofanyika nchini sababu kubwa inayochangia vifo vya mama na mtoto ilionekana kuwa ni kupitia ucheleweshwaji wa aina tatu. Kwanza ni ngazi ya jamii kufanya maamuzi sahihi kwa wakati kufika katika vituo vya kutolea huduma za afya. Pili ilikuwa ni njia au miundombinu ya kumfikisha katika vituo vya kutolea huduma za afya. Tatu ni kwenye vituo vyenyewe vya utoaji huduma za afya wanakofika, mama anakuta wateja ni wengi wanaohitaji huduma, vitendea kazi kuwa vichache wakiwemo wahudumu wenyewe, vitengo mbalimbali vikiwemo vya kufanyia upasuaji na mazingira mengine. Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Dkt. Jesca Lebba na kutoa wito kwa Redio za jamii kusaidia kuelimisha umma juu ya mfumo wa M-Mama unaotoa fursa ya usafiri wa dharula kwa Mama na Mtoto mchanga kuanzia kwenye ngazi ya jamii hadi kwenye vituo vya kutolea huduma wakati wa dharula.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.