NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Serikali Wilayani Kibaha imeipongeza kwa dhati uongozi wa Halmashauri ya mji Kibaha kwa kuweka mikakati madhubuti ya kuongeza wigo kwa ajili ya kuweza kukusanya fedha kutokana na mapato ya ndani ambazo zimekwenda kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John wakati wa kikao cha ushauri cha Halmashauri ya Kibaha mji kilicholenga kuwakutanisha watendaji, wataalamu, wakuu wa idara, viongozi wa dini pamoja na vyama vya siasa kwa lengo la kujadili mambo mbali mbali ikiwa pamoja na kutoa ushauri ambao utaweza kusaidia katika kutatua kero na changamoto ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi.
Mkuu huyo alisema kwamba kupitia mapato ya ndani Halmashauri ya mji Kibaha imeweza kujitahidi kwa hali na mali kutengeneza madawati yapatayo 4000 katika shule mbali mbali ambayo yataweza kuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi kuondokana na changamoto ya kusoma kwa mlundikano mkubwa.
Kadhalika Mkuu huyo wa Wilaya ameweza kuongeza kuwa katika mapato ya ndani wameweza kupeleka kiasi cha shilingi milioni ambazo zimekwenda katika kila kata kwa lengo la kuboresha miundombinu ya barabara ili ziweze kupitika kwa urahisi katika kipindi chote na wananchi waondokane na kero hasa katika kipindi cha mvua.
Pia katika hatua nyingine alisema kuwa Halmashauri ya mji Kibaha wameweza kununua gari mpya kupitia mapato ya ndani ambayo itaweza kurahisisha ufanisi kwa watumishi na wataalamu kutekeleza majukumu yao kwa urahisi, sambamaba na kubuni mradi wa kupaki magari makubwa ambayo itakuwa ni fursa ya kipekee kujiongezea kiwango cha mapato.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmasshauri ya mji Kibaha Dkt.Rogers
Shemwelekwa amesema kwamba wametumia kiasi cha shilingi bilioni 8 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wa soko kubwa la kisasa ambalo limejengwa kutokana na fedha ambazo zimetolewa na Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuweza kuwasogezea huduma wananchi kwa urahisi.
Alisema kwamba soko hilo la kisasa litakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Kibaha pamoja na maeneo mengine ya jirani kutokana na kuwepo kwa bidhaa mbali mbali zilizomo katika soko hilo la kisasa ambalo limejengwa katika kiwango kikubwa ambapo litaweza kuwapunguzia wananchi kwenda umbari mrefu kwa ajili ya kuweza kupata mahitaji yao mbali mbali.
Dkt. Rogers amempongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo kiais cha shilingi bilioni nane ambazo ndizo zimeweza kufanikisha kwa kiasi kikubwa kukamilika kwa mradi wa ujenzi huo wa soko la kisasa ambalo litataweza kuwa ni chachu kubwa ya kuleta maendeleo ya kukuza uchumi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.