ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 4, 2024

CCM NYAMAGANA WAFANYA SHEREHE BAADA YA KUSEPA NA MITAA 172 KATI YA 175 UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Hatoki mtu haingii mtoto wala, mtoto hatumwi dukani, hivi ndivyo ilivyokuwa Jumamosi ya tarehe 30 Novemba 2024, jijini Mwanza mara baada ya wanachama na wadau wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Nyamagana kufanya matembezi yao ya amani kusherehekea ushindi wa kishindo walioupata katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuchaguwa wenyevititi na wajumbe wawakilishi kwa mahudhurio makubwa yasiyo na mfano. Kati ya mitaa 175, CCM imesepa na mitaa 172 ikiacha mitatu tu kumilikiwa na upinzani, rubani wa kusanyiko hili Peter Bega ambaye ni mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana baada ya kuwasili katika viwanja vya Kemondo garden, yeye na wanachama wote wanajikabidhi kwa mwenyezi Mungu. Swali linabaki - sasa jeh CCM itafanyaje kazi na hawa wenyeviti watendaji waliochaguliwa kutoka upinzani, jeh itakuwa ni figisu za kosa ukose wewe, mimi nipate sifa au pengine itakuwa ni siasa za mizengwe yenye vuta nikuvute?

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.