ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 4, 2024

WAWILI MWANZA WAJISHINDIA BAJAJI ZA MIZIGO KUTOKA 'BONGE LA MPANGO' LA NMB.

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Pancras Hassan na Deogratius Joseph Kisoka mfanyabishara na mkazi wa Mahina wilayani Nyamagana jijini Mwanza, ni washindi wawili waliojishindia pikipiki ya magurudumu matatu kila mmoja na kukabidhiwa papo hapo na Mkuu wa Matawi na Mauzo NMB, Donatus Richard. ............................................................................................................................ Katika kuhamasisha utamaduni wa watanzania kujiwekea akiba ili kukabiliana na dharura zinazoweza kujitokeza za uhitaji wa fedha, Benki ya NMB imetoa zawadi kwa wateja wake kupitia kampeni ya ‘Bonge la Mpango, mchongo ndio huu’. Zawadi hizo zimetokana na washindi wa bahati nasibu inayochezeshwa na benki hiyo kwa wateja wake waliojiwekea akiba ya kuanzia shilingi 100,000 na kuendelea. Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo, Mkuu wa Matawi na Mauzo NMB, Donatus Richard amesema kampeni hiyo ya kila mwaka ya ‘Bonge la Mpango’ inalenga kuhamasisha watu kufungua akaunti na kujiwekea akiba ili kutatua matatizo ya dharura yanayohitaji fedha . Amesema zawadi wanazotoa kwenye kampeni hiyo ya kila mwaka inayodumu kwa miezi 12 ni pamoja na kitita cha shilingi milioni 100 kila mwaka, 100,000 kila wiki, friji, TV, pikipiki ya magurudumu mawili (Toyo) na pikipiki ya magurudumu matatu (Guta na Bajaji sambamba na mashine ya kufulia,majiko ya Gesi, trekta za kilimo (Power tiller).

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.