ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 29, 2024

MV MWANZA HAPA KAZI TU YAFIKIA ASILIMIA 96 KUANZA SAFARI ZAKE AFRIKA MASHARIKI HIVI KARIBUNI

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Meli Mpya ya kubeba Abiria na Mizigo ya MV Mwanza hapa kazi tu, kwa mara ya nyingine imefanya safari ya majaribio ya kiufundi katika Ziwa Victoria. Mara baada ya majaribio ya siku 3, Waziri wa Uchukuzi Makame Mbarawa anaongoza zoezi la ukaguzi wa Mv Mwanza Hapa Kazi Tu, iliyoondoka katika Bandari ya Mwanza Kusini ikiwa na jopo la wadau, wakiwemo Wahandisi, Wakandarasi, Wandishi wa Habari pamoja na Wataalam waliokuwa wakiijenga meli hiyo. Eric Hamisi ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Nchini na hapa anaeleza zaidi ni yapi yaliyosalia kwa ujenzi wa meli hiyo ili kuanza safari zake. Meneja Mradi wa Ujenzi wa Meli ya MV. Mwanza hapa kazi tu Vitus Mapunda amesema majaribio hayo ni ishara ya kukamilika kwa Ujenzi wa Meli hiyo, nao wakiwa na dhamana ya kuilinda na kuitunza. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya huduma za Meli MSCL Meja Jenerali Mstaafu John Mbungo amesema Watanzania wanapaswa kuona fahari kubwa ya ushiriki wao katika Ujenzi wa Meli hiyo. Wakazi wa Jiji la Mwanza wameipongeza Serikali kwa kukamilisha Ujenzi wa Meli hiyo. Meli ya MV. Mwanza hapa kazi tu yenye uwezo wa kubeba Abiria 1,200, Tani 400 za Mizigo, si chini ya Magari Madogo 28 na Malori Matatu unatarajiwa kukamilika ndani ya Mwaka huu ambapo Ujenzi wake ulianza Mwaka 2019 ukitekelezwa na Mkandarasi kutoka Korea ya Kusini zikishirikiana na Suma JKT ya Tanzania, Mradi huo umegharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 127 za Kitanzania.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.