Mwanamke mmoja raia wa Nigeria amejawa na machozi baada ya mchumba wake kufuta harusi yao.
Mrembo huyo alianika
suala hilo kwenye kundi la Facebook na kuomba ushauri wa wanamtandao.
Alisema alimtembelea tu
mpenzi wake wa zamani ili kumpa kadi ya mwaliko kwenye harusi yake, lakini
aliishia kurusha roho na jamaa huyo.
Kwa bahati mbaya, mume
wake mtarajiwa aligundua kuhusu uzinzi wake baada ya kudukua simu yake.
Baadaye mwanamume huyo
aliagiza kwamba matayarisho yote ya harusi yasitishwe mara moja.
Mrembo huyo alilalama
kuwa: "Mbele yangu, aliwaita wazazi wote wawili na kuwataka wasitishe
maandalizi yote ya harusi.
Walipouliza kwanini,
aliwaambia nitaeleza vizuri zaidi. Aliniacha nyumbani kwake na kwenda hotelini
na hakurudi"
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.