Afisa wa Polisi kutoka Kaunti Ndogo ya Khwisero, Kaunti ya Kakamega anakabiliwa na tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato cha kwanza mwenye umri wa miaka 16 akiwa kizuizini.
Kulingana na ripoti,
tukio hilo linaripotiwa kutokea katika Kituo cha Polisi cha Khwisero.
Msichana huyo
alikamatwa Aprili 28, 2023, pamoja na rafiki yake ambaye alikuwa ameambatana
naye kumuona mpenzi wake.
Wazazi wao walikuwa wamewaomba polisi
kuwakamata na kuwatupa kwenye seli kama adhabu.
Hata hivyo, inadaiwa
polisi huyo alikwenda katika chumba walichokuwa wamewafungiwa wasichana hao na kumtaka
mwathiriwa amfuate katika chumba kingine, ambapo alimuamuru kuvua nguo.
Inadaiwa kuwa afisa
huyo alimnajisi mtoto huyo akirudia kwa kutumia kondomu
Afisa huyo, kulingana
na Vivian Ayuma, mkurugenzi wa huduma za kijamii, huduma za watoto, utamaduni
na jinsia katika kaunti hiyo, bado hajakamatwa.
Hili ni jambo la
kusikitisha sana ambalo limefungwa chini ya kapeti.
Tunaomba uchunguzi
kamili ufanyike kuhusu tukio hili la kusikitisha.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.