Katika tukio tofauti, maafisa wawili wa polisi wameuawa na umati wenye hasira katika soko la Kanthanje, Chuka kwa wizi.
Akithibitisha kisa hicho, kamanda wa polisi wa
Kaunti ya Tharaka Nithi Zacheus Ng’eno, alisema kuwa wawili hao walipigwa hadi
kufa na umati wa watu baada ya mayowe ya mmiliki wa duka la M-Pesa kuvutia
watu.
Mfanyabiashara huyo
alipiga nduru akidai kuvamiwa na watu wanaoshukiwa kuwa majambazi kutoka ndani
ya duka lake mwendo wa saa nane usiku wa kuamkia Jumamosi, Aprili 29.
Umati ulijibu kwa haraka kamsa hizo na
kuchukua hatua ambayo ilisababisha vifo vya maafisa hao wawili wa polisi ambao
wanasemekana walikuwa wamevalia nguo za raia wakati wa tukio hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.