Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani limezifungia vyuo vya mafunzo ya udereva 161 kutokana na kukosa sifa ya kutoa mafunzo hayo.
Kupitia taarifa iliyotolewa na jeshi hilo,
vyuo hivyo vilibainika baada ya ukaguzi walioufanya kuanzia Machi mosi hadi
April 29, 2023.
Kulingana na taarifa hiyo ya Jeshi la Polisi,
kufuatia uhakiki wa leseni uliofanyika Machi mosi hadi April 29 mwaka huu,
madereva waliosajiliwa wenye leseni C na E ni milioni 1.59 huku
leseni 20,944 zikiwa zimehakikiwa.
Kati ya hizo leseni 17,726 za madereva
zimebainika kuwa na sifa na wamepewa barua ya udhibitisho, leseni 3,214
zimefutiwa madaraja kwani madereva wa leseni hizo hawana sifa ya kuwa na madaraja
C na E kutokana na kutosomea madaraja stahiki,"imesema taarifa hiyo
Pia, taarifa hiyo imebainisha kwamba kwa
upande wa uhakiki wa vyuo vinavyotoa mafunzo ya udereva vilivyoanza Januari
mwaka huu hadi April ilibainika ni vyuo 134 pekee ndio vyenye sifa kati ya 297,
Vyuo 161 vikibainika kutokidhi vigezo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa shule ya
udereva ya Pachoto, Juma Manguya amesema shule hiyo ilipewa kibali cha kutoa
mafunzo ya fani hiyo na jeshi hilo tangu mwaka 2018 lakini anashangaa kufungiwa
kwa madai hakina sifa.
Nimeshangaa kuona kupitia operesheni
waliyoianzisha wanafuta vyeti vilivyotolewa na shule yangu wakati jeshi
liliruhusu siyo jambo jema ni muhimu wakaangalia upya suala hili Kwa sababu
watu waliwekeza muda wao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.