Kundi kubwa la mbuzi wakorofi wenye tabia ya kuzurura katikati ya mji nchini Uingereza wameachiliwa huru baada ya kushinda kesi ya uzururaji.
Mbuzi hao wamekuwa wakizurura mitaani kwa zaidi
ya miaka 100 wakiwa na tabia mbovu za kula mimea na uzio wa nyumba za watu.
Isitoshe, mbuzi hao wenye pembe ndefu waliingia kwenye hoteli, wakipanga foleni nje ya nyumba ya utunzaji wakati wa chakula cha jioni wakitarajia chakula na kutembelea kituo cha huduma cha ndani.
Baraza la
Halmashauri ya Llandudno, North Wales iliamuru mbuzi hao kuachiliwa licha ya
tabia zao mbovu, likisema ni jukumu la wamiliki wa ardhi kulinda mali zao
kutoka kwa genge la wanyama hao badala ya kuzuiliwa, Daily Star limeripoti.
Hata hivyo,
pendekezo hilo lilikataliwa kufuatia maandamano makubwa ya umma mjini
Bodlondeb.
Mbuzi hao
walipata umaarufu mwaka wa 2020 walipovamia mitaa iliyoachwa tupu wakati wa
janga la kimataifa la COVID-19.
Zaidi ya
mbuzi 200 huondoka mara kwa mara kwenye eneo la Orme Mkuu kurandaranda mitaani.
Kwa mujibu
wa ripoti ya Baraza la Halmashauri, hakuna mtu au shirika moja ambalo
linawajibika kisheria kwa idadi ya mbuzi hao ambao Malkia Victoria alitoa kama
zawadi kwa kiongozi wa eneo hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.