Mwanamke mmoja (jina limehifadhiwa) jijini Nairobi nchini Kenya ameshtakiwa kwa kosa la kula njama ya kumuuza mjukuu wake kwa Sh400,000 ya nchini humo (Sh6.9 milioni).
Mwanamke
huyo mwenye miaka 39 alikamatwa Aprili 9, 2023 na polisi ambao walijifanya wana
nia ya kumnunua mtoto huyo mdogo mwenye siku tano.
Kwa
mujibu wa gazeti la Daily Nation la nchini humo limeripoti kuwa mtuhumiwa huyo
alimchumkua mjukuu wake Kaunti ya Kakamega baada ya mtoto wake mwenye umri wa
miaka 16 kujifungua na kumtaka akamlee mjini Nairobi ili binti yake aendelee na
masomo.
Baada
ya kufika Nairobi, mwanamke huyo alianza kutafuta mteja wa kumuuzia mtoto huyo
kabla hajatiwa mikononi mwa polisi
“Walipanga
kukutana kwenye mgahawa mmoja jijini Nairobi na hatimaye kuwakamata, wakamwokoa
mtoto huyo na kumpeleka kwenye kituo cha kulelea watoto,” tovuti ya Daily
Nation imeripoti.
Mshukiwa
huyo yupo rumande tangu akamatwe baada ya polisi kupata agizo hilo kutoka
mahakamani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.