Wanawake wawili wamempiga na kumuua kaka yao kufuatia ugomvi wa chakula katika kaunti ya Bungoma.
Katika
kisa hicho cha Jumanne - Machi 28 - usiku, wanawake hao wanaripotiwa kugombana
na kaka yao kuhusu chakula na ugomvi huo kufika kiwango cha kupigana.
Akithibitisha
kisa hicho, Kamanda wa Polisi wa Webuye Mashariki Irene Kerubo alisema kuwa
siku huyo, mwanamume huyo ambaye hakuwa ameoa, alirejea nyumbani mwendo wa saa
tano usiku na kuanza kuagiza chakula kutoka kwa dada zake.
Baba wa watatu hao - Shadrack Mukoyani,
amesema kuwa huenda ombi la mwanawe wa
kiume kuwaomba chakula kwa nguvu.
liliwazingua dada zake ambao sasa wamekamatwa na
polisi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.