Na Victor Masangu,Kibaha
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvesty Koka katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita katika kuleta chachu ya maendeleo ameamua kutumia fedha za mfuko wa Jimbo kwa ajili ya kuboesha sekta ya elimu na afya katika kata zilizopo pembezo mwa mji.
Hayo yamebaibika wakati wa ziara ya kikazi kwa ajili ya kukagua na kutembelea miradi mbali mbali ambayo imetekelezwa kwa kutumia fedha za mfuko wa jimbo katika sekta mbali mbali ikiwemo miradi ya elimu pamoja na afya.
Katika ziara hiyo Mbunge huyo ameambatana na wajumbe wa kamati ya mfuko wa Jimbo alisema lengo lake kubwa la kufa ya ziara hiyo ni kuweza kujionea jinsi ya utekelezaji wa miradi hiyo ambayo inatekelezwa kwa fedha za mfuko wa Jimbo.
Aidha Koka alisema kwamba ataendelea kushirikiana bega kwa bega na wananchi katika kusikiliza kero na changamoto ili kuweza kuzisikiliza na kuzitafutia ufumbuzi lengo ikiwa ni kuwaletea mabadiliko chanya ya kimaendelea katika nyanja mbali mbali.
" Nia yangu kubwa ni kuwaletea maendeleo wananchi wangu wa Jimbo la Kibaha mji,na ujio huu kikubwa ni kikagua fedha ambazo nimezitoa za mfuko wa Jimbo zimefanya kazi yake ipasavyo na ndio maana nimeamua kufanya ziara hii ili nione miradi imetekelezwa katika kiwango,"alisema Koka.
Pia aliongeza kuwa anataka kuona kata zilizopo pembezo zinapiga hatua kubwa ya kimaendeleo na ataendelea kuwapambania wananchi wake ili waweze kupata fursa ya kupata huduma mbali mbali za kijamii.
Katika hatua nyingine aliwataka watendaji Kuhakikisha wanaweka mipango madhubuti ya kutenga maeneo maalum ambayo yataweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kutumika kwa miradi ya maendeo kwa wananchi.
Kwa Upande wao baadhi Diwani wa kata ya Mbwawa pamoja na diwani wa kata ya Visiga wamemshukuru Mbunge huyo kwa kutenga fedha za mfuko wa Jimbo kwa ajili ya maendeleo kwa wananchi wake.
Naye mkuu wa shule ya sekondari misugusugu Mohamed Mwenda alisema juhudi ambazo zimefanyika na Mbunge katika kusaidia viti 30 na meza 30 vimeweza kuwa mkombozi mkubwa katika kusaidia wanafunzi kuondokana na adha ya kukaa kwa msongamano.
Nao baadhi ya wazazi na walezi wakiwemo viongozi wa chama wamempongeza Mbunge huyo kwa kuwapambania kuleta chachu ya maendeleo katika sekta mbali mbali pamoja na kutumia fedha za mfuko wa Jimbo katika miradi ya maendeleo.
Mbunge koka amefanya ziara ya kishindo katika kata sita za Mbwawa.Visiga.Misugusugu,Kibaha,viziwaziwa pamoja na Kibaha kwa ajili kutembelea miradi mbali mbali ambayo baadhi yake imetekelezwa kwa kutumia fedha za mfuko wa jimbo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.