Serikali ya Italia yapania kuanzisha sheria ya kuwatoza faini raia wake watakaotumia maneno ya Kiingereza au lugha nyingine yoyote ya kigeni katika mawasiliano au nyaraka rasmi.
Sheria hiyo mpya sasa itawataka Waitaliano wote
wanaofanya kazi kwenye idara za umma kuwa na uwezo wa kusoma, kuandika na
kukimudu Kiitaliano
Wale watakaoenda kinyume na sheria hiyo watalipa
faini ambayo inaweza kufikia kiasi cha zaidi ya euro 100,000(254,954,420.30 tsh).Japo
sheria hiyo inajumuisha lugha zote za kigeni, hata hivyo Kiingereza ndiyo
inalengwa zaidi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama cha
Brothers of Italy ambao ndio waanzilishi wa muswada huo, matumizi ya maneno ya
Kiingereza yanakidhalilisha na kukishushia hadhi Kiitaliano.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.