Dar es Salaam. Watu ambao idadi yao haijafahamika wakiwemo wanafunzi, wamenusurika kifo baada ya daladala kufeli breki kisha kugonga magari mengine mawili njia panda ya Goba jijini Dar es Salaam kisha kuanguka.
Ajali hiyo imetoke leo Jumanne Novemba 22, 2022 ikiwa ni siku chache tangu lori aina ya Scania kugonga magari madogo saba na kusababisha kifo cha mtu mmoja pamoja na majeruhi wawili eneo la Tegeta njiapanda ya Wazo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mtatiro Kitinkwi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusababisha majeruhi tisa wengi wao wakiwa wanafunzi.
Kitinkwi amesema, saa moja kasoro asubuhi, gari moja liligonga gari namba Coster iliyokuwa inaendeshwa na Venance Silvester (44), mkazi wa Tegeta.
"Baada ya kugonga gari hilo pia liligonga gari lingine Scania lililokuwa likiendeshwa na Bakhar Barhan (43) lililokuwa linatoka Tegeta kwenda Mwenge," amesema Kamanda Kitinkwi.
Amesema Jeshi hilo linaendelea kuchunguza chanzo cha ajali hiyo, baadabya dereva kukimbia, tayari majeruhi wanaendelea matibabu na hali zao zinaeendele vizuri baada ya wanafunzi wanne kuruhusiwa.
Baadhi ya mashuhuda wameeleza, ajali hiyo imetokea baada ya gari kufeli breki wakati linatokea Goba kwenda Kawe.
"Dereva alijitahidi, tangu mteremko wa Goba lakini ilipofika njia panda aligonga lori ubavuni kisha kupinduka," amesema
"Ilikuwa ikiteremka kwa kasi na wanafunzi wakipiga kelele wengine wakijaribu kuruka, baada ya kuruka tuta liliongeza kasi na kwenda kuligonga lori ubavuni na kuanguka," amesema Nehemia John shuhuda wa ajali hiyo.
Dereva bodaboda, Imani Mushi alisema aliona gari hilo likiwa kwenye kasi na kusikia kishindo, likawa limegonga lori na kuanguka ndipo walipoanza kuokoa majeruhi.
Mzazi wa Khairath Ismail (12), mwanafunzi wa shule ya msingi Kawe amesema alipigiwa simu na mtu aliyekuwa anamfahamu, baada yakumuona akiingizwa katika hospitali ya Massana.
"Nilipata mshtuko mkubwa, baada ya kupata taarifa hizi nilipokuja nilimkuta mwanagu kavunjika, nashukuru yuko salama tunafanya taratibu za kumuhamishia hospital ya Taifa Muhimbili (MNH) kwaajili ya vipimo zaidi," alisema Ismail.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.