Mke wa zamani wa Bill Gates Melinda yuko kwenye uhusiano mpya wa mapenzi mwaka mmoja baada ya kukamilisha talaka yake na bilionea huyo.
Hapo awali Melinda aliolewa na Bill Gates, lakini walitalikiana rasmi mnamo Agosti 2021.
Bill na Melinda waliushangaza ulimwengu walipotangaza kuwa wanaachana rasmi baada ya kuishi kwenye ndoa kwa miaka 27.
Wengi walijiuliza ni nini kilisababisha wawili hao kutengana, huku wengine wakisema kuwa kweli pesa haziwezi kununua mapenzi.
Wengi walikuwa na wasiwasi kuhusu jinsi talaka ya wawili hao ingeathiri mamia ya miradi ulimwenguni ambayo walianzisha pamoja.
Hata hivyo, kwa mujibu wa TMZ, Melinda kwa sasa anachumbiana na mara kwa mara amekuwa akionekana na aliyekuwa mwandishi wa habari kwenye Televisheni anayedaiwa kuwa mpenzi wake.
Duru zinaarifu kwamba Melinda amekuwa akichumbiana na Jon Du Pre kwa miezi michache au hata zaidi ikizangatiwa nyakati ambazo wameonekana pamoja.Mke wa zamani wa bilionea huyo alionekana akiwa na mwandishi huyo kwenye mechi ya mpira wa vikapu mnamo mwezi wa Aprili, swala lililowaacha wengi na masali chungu nzima.
Ingawa hakuna anayejua jinsi walivyokutana kwa mara ya kwanza, kilicho wazi ni kwamba wawili hao na baadhi ya jamaa zao hivi majuzi walikuwa na likizo ya pamoja.
Melinda alifanya mahojiano yake ya kwanza tangu yeye na bilionea wake wa zamani walipotengana mapema mwaka huu, na alizungumzia jinsi ilivyoathiri maisha yake.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 58 alisema alifikia hatua katika ndoa yake hakuweza kuvumilia tena na ikabidi aondoke kwa sababu ilikuwa imeingia doa.
Aliongeza kuwa roho yake inapona na alihisi kwamba anafungua ukurasa mpya huku akisubiri kuona jinsi siku zilizoko usoni mwake zitakavyokuwa. .
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.