YANGA wameandika historia kwa kupata ushindi ugenini na kutinga hatua ya makundi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
Ushindi pekee umepatikana kipindi cha pili kupitia kwa kiungo wa Yanga Aziz KI ambaye alianzia benchi kwenye mchezo wa leo.
Dakika 45 za awali ni beki Kibwana Shomar alikuwa ni mwiba kwa wapinzani wao Club Africain ambapo alipiga mashuti mawili ambayo yalilenga lango.
Kiungo Bernard Morrison na Sure Boy walikuwa na kazi kubwa uchezesha timu ya Yanga iliyocheza soka la pasi nyingi kipindi cha kwanza na cha pili.
Bao la ushindi limepachikwa dakika ya 79 kwa nyota huyo kuwatungua Waarabu wa Tunisia kwa shuti lilimshinda mlinda mlango baada ya kupokea pasi ya kichwa kutoka kwa mshambuliaji wao mahiri Fiston Mayele.
Pongezi kwa kipa namba moja wa Yanga, Diarra Djigui ambaye alifanya kazi kubwa kuwakikisha anaweka mazingira ya lango lake linakuwa salama kwa dakika zote.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.