ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 9, 2022

ALIYEFARIKI AJALI YA NDEGE AZIKWA SIKU YA BIRTHDAY YAKE.

 

Enzi za uhai wake Zaituni Mohamed Shillah.

SIMANZI na majonzi vimetawala katika mazishi ya mmoja kati ya abiria 19 waliofariki katika ajali ya ndege iliyotokea Ziwa Victoria mkoani Kagera, Zaituni Mohamed Shillah (28), ambaye amezikwa tarehe ambayo inafanana na siku aliyozaliwa.

Leo Jumatano Novemba 9, 2022 tofauti na misiba mingine ulinzi ulikuwa umeimarishwa na ilikuwa marufuku kupiga picha wala kurekodi tukio lolote.

Familia hiyo ilikumbwa na majonzi kwani leo Zaituni alitarajia kusherekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa ambapo alizaliwa Novemba 9, 1994, mkoani Dodoma.

Ibada ya mazishi ya Zaituni imeongozwa na Mchungaji Loserian Kambei wa Kanisa la The Mountain Hebron Ministry.


Marehemu ambaye alikuwa akifanya kazi jijini Dar es Salaam na alikuwa anakwenda kikazi mkoani Kagera hata hivyo hakuna aliyekuwa tayari kueleza sehemu aliyokuwa anafanya kazi.


Katika ibada hiyo iliyofanyika nyumbani kwa Idd wilayani Arumeru kabla ya kwenda kuzikwa katika eneo la TPRI, ilihudhuriwa na watu wachache.


Katibu Tawala wa Wilaya  ya Arumeru, James Mchembe, aliongoza waombolezaji katika mazishi hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Suleiman Msumi, kamati ya ulinzi na usalama na ndugu na jamaa wa karibu wa familia hiyo.


Zaituni ambaye alizaliwa mkoani Dodoma Novemba 9, 2022, alikuwa akijishughulisha na kazi ya ofisa masoko wa kidigitali jijini Dar es Salaam.


Akihubiri katika ibada hiyo ya maziko, Mchungaji Kambei, amesema ajali hiyo imekuwa pigo kubwa kwa taifa kwani imepoteza nguvu kazi ambayo ilikuwa ikitegemewa


Kuhusu vijana alisema ni wakati wa jamii na taifa kwa ujumla kuombea kundi la vijana ambalo kwa asilimia kubwa wamekiuka maadili na kujihusisha na vitendo viovu.


"Tunalia kama kanisa, watu wanapenda anasa kuliko Mungu,vijana wanajishughulisha na matukio ya ajabu ikiwemo panya road,taifa linaelekea wapi?"Wazazi tuombe kwa ajili ya vijana,watu wamejisahau, tunalia juu ya vijana ni lazima kama jamii tukemee vitendo viovu kwani kizazi kinaangamia,msiba huu ni huzuni kwani leo tunamzika Zaituni na ingekuwa maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa,"aliongeza


Kuhusu mvuvi Jackson Majaliwa, ambaye aliokoa manusura wa ajali hiyo ambaye alitumia kasia kuufungua mlango wa ndege  na kuwezesha watu 24 kuokolewa, amesema ni muhimu jamii kuhakikisha inatenda mema na kusaidiana bila kujali hali zao.


"Jiulize kijana aliyefanya uokoaji ni kijana ni mdogo sana inawezekana alikuwa anatamani kuwa jeshi la uokoaji,lakini hakupata nafasi hiyo.Watu wanalia,yeye imekuwa fursa kwake dunia inamjua leo kwa alichokifanya,labda alikata tamaa lakini Mungu amemsaidia,"amesema

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.