Azma ya mgombea wa Azimio la Umoja One Kenya Alliance Raila Odinga kufika Ikulu ya kwa mara nyingine tena imegonga mwamba.
Raila alibwagwa na mpinzani wake mkuu wa kisiasa wa Muungano wa Kenya Kwanza William Ruto katika uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkubwa uliofanyika Jumanne, Agosti 9.
Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati, Ruto alipata kura 7,176,141 ikiwa ni asilimia 50.49 ya kura zote zilizojumlishwa za kutangazwa mshindi. Waziri Mkuu huyo wa zamani aliibuka wa pili kwa kura 6,942,930 akiwakilisha 48% ya kura zote zilizojumlishwa.
Hili ilikuwa ni mara ya tano kwa kiongozi huyo wa ODM kupigania kiti hicho cha urais bila kufaulu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.