Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kijiji cha Saadan Kuwa Mwenge wa Uhuru Unaweza Kwenda Kuweka Jiwe la Msingi Katika ujenzi wa Bwawa Hilo
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo kuhusu ujio wa Mwenge wa Uhuru katika kijiji cha Saadan Kwenda Kuweka Jiwe la Msingi Katika ujenzi wa Bwawa Hilo
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MKUU wa wilaya ya Iringa Mohamed
Hassan Moyo amesema kuwa mwenge wa Uhuru utaweka jiwe la msingi katika mradi wa
ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika Kijiji cha Sadan kata ya
Masaka unaosimamiwa na uongozi wa Bonde la Rufiji.
Akizungumza wakati wa ziara ya
waziri wa maji Juma Aweso alisema kuwa mradi huo wa ujenzi wa bwawa la
kuhifadhia maji ya mvua ni mradi mkubwa na ambao unasimamiwa kwa ubora
unatakiwa hivyo anaenda kuitarifu kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya
Iringa ili kufanikisha mwenge wa Uhuru utaweka jiwe la msingi.
Moyo alisema kuwa serikali ya
awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kupitia wizara ya maji imetoa fedha nyingi
katika mradi huo hivyo unapaswa kupewa hadhi ya kitaifa kwa kuwa unaenda
kutatua changamoto za wananchi wa kata ya Masaka na kata nyingine za jirani.
Akiwa katika ziara wilaya ya
Iringa waziri waji Juma Aweso ameupongeza uongozi wa wilaya ya Iringa kwa
kusimamia vizuri ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika bodi ya maji
Bonde la Rufiji kwa kuwa litafanikisha kuleta maendeleo kwa wananchi na kutatua
changamoto ya maji kwa wananchi wa kata ya Masaka.
Aweso alisema kuwa ameridhishwa
na ujenzi wa mradi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika Kijiji cha Sadan
kwa kuwa mmoja ya miradi mingi mikubwa ambayo itakuja kuwa na matokeo ya moja
kwa moja kwa wananchi wanaolizunguka bwawa hilo.
Aweso alisema kuwa serikali ya
awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imeiagiza wizara ya maji kuhakikisha inachimba
mabwawa ya kila wilaya ili kutatua changamoto hiyo na kuongeza njia za kukuza
uchumi wa maeneo husika.
Alisema kuwa kukamilika kwa bwawa
hilo kutaisaidia kuleta maendeleo ya miradi mingine ya maji kutokana na
usimamizi mzuri ambao unafanywa na uongozi wa wilaya na mkoa kwa ujumla kwenye
maendeleo ya miradi ya kijamii.
Alisema mradi huo wa ujenzi wa
bwawa la kuhifadhia maji ya mvua utagharimu kiasi kikubwa cha fedha ambacho ni
900,982,000/= ambazo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amezileta
kutatua changamoto hizo kwa wananchi wa kata ya Masaka.
Aweso alisema kuwa wizara ya maji
musimu huu wa kiangazi inajenga mabwawa kumi (10)ambapo mabwawa manne
(4)yanajengwa katika wilaya ya chemba,mawili wilaya ya Bahi,wawili wilaya ya
Chamwino na wilaya ya Iringa mabwawa mawili na wizara inafanya usanifu wa
mabwawa 51 ambayo yanatarajiwa kujengwa katika mwaka ujao wa fedha
Awali akisoma taarifa ya mradi
kwa waziri,msimamizi wa mradi huo Eng Geofrey Simkonda alisema kuwa mradi wa
ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua ni mkakati wa
uendelezaji,utumiaji,uhifadhi na usimamizi wa vyanzo vya maji katika Bonde la
Rufiji.
Alisema kuwa lengo la ujenzi wa
mradi huo wa ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua ni kuvunia maji na
kurahisiha upatikanaji wa maji kwa wananchi hususani wenye uhaba wa rasilimali
za maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya kibinadamu.
Eng Simkonda alisema kuwa
wananchi wa wilaya ya Iringa,kata ya Masaka inayojumuisha Vijiji vya Makota,
Sadan na Kaning'ombe watanufaika na mradi huo.
Alisema kuwa bwawa la kuhifadhia
maji ya mvua la Masaka lina kimo cha mita 14,urefu mita 260 na litakuwa na
ujazo wa mita 439,803 na ujenzi unatarajiwa kukamilika mwezi wa tisa mwaka 2022
hadi sasa mradi umefikia asilimia 50.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.