Mwanamke mmoja mkazi wa Kitongoji cha Kililangwena wilayani Tanganyika mkoani Katavi, Fadhia anatuhumiwa kumuua mumewe Laurent Buchumi (36) kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali shingoni.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ally Makame amesema tukio hilo limetokea Machi 24, 2022 saa 5:30 usiku nyumbani kwa wanandoa hao baada ya kutokea ugomvi baina yao.
“Walikuwa na ugomvi ndani, baada ya kutokea ugomvi mwanaume alitoka nje na mtuhumiwa alimfuataa na kumchoma na kitu chenye ncha kali” amesema
Mbali na hilo Kamanda Makame amesema Belta Fransisco mkazi wa mtaa wa Ilembo Manispaa ya Mpanda ameua kwa kupigwa na kitu kizito chenye ncha kali kichwani kwake alipokuwa shambani.
Kamanda Makame ameeleza kuwa tukio hilo limetokea Machi 24 saa 3:30 asubuhi shambani kwake.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.