WATOTO 892 wafanyiwa ukatili kwa muda wa mwaka mmoja katika wilaya ya Ileje mkoani Songwe na kupelekea kuhatarisha maisha yao ikiwa ni pamoja na kukosa haki yao ya kupata elimu.
Hayo yamethibitishwa na Afisa Ustawi wa jamii wa wilaya hiyo Methew Meisha alipozungumza na mwandishi wa gazeti hili, kwa kudai kuwa Wilaya ya Ileje matukio ya unyanyasaji yamekuwa yakiongezeka kila mwaka na kuhatarisha ujenzi wa jamii bora kwa baadae.
Meisha aliyabainisha matukio yaliyokithiri kwa Ileje kuwa ni pamoja na ukitili wa Kingono, ukatili wa kimwili (kuchomwa na na kupigwa), ukatili wa kihisia na ukatili wa kutelekezwa watoto wadogo chini ya miaka mitano (5).
Alisema katika kipindi cha mwaka 2019 na 2020 jumla ya watoto 892 katika wilaya hiyo wamefanyiwa ukatili, huku akitanabaisha kuwa ukatili wa kingono ndio uliokithiri zaidi kwa kuwa na idadi kubwa ya watoto waliofanyiwa ukatili.
Alitaja takwimu hizo kuwa jumla ya watoto 50 walifanyiwa ukatili wa kimwili kwa mawaka 2019 wakike wakiwa 28 na wakiume 22, watoto 122 walifanyiwa ukatili wa Kingono (kubakwa na kulawitiwa wakike wakiwa 89 na wakiume 33 na ukatili wa kihisia (madhara kiakili) watoto 196 wakike 121 wakiume 77.
Ukatili wa kutelekezwa (bila msaada ,mahitaji) watoto chini ya miaka mitano wataoto 77 walitelekezwa wakike 46 na wakiume 31.
“kwa msimu wa 2020 takwimu ziliongezeka ambapo watoto 151 walifanyiwa ukatili wa kimwili kupigwa na kuchomwa , wakike 120 na wakiume 31, uktili wa kingono na ulawiti watoto 127, wakike 124 na watoto watatu wa kiume walilawitiwa.
Ukatili wa kihisia (madhara kiakili) watoto 532 walifanyiwa ,wakike 401 na kiume 131, kwa uopande wa ukatili wa kutelekezwa (bila msaada na mahitaji watoto chini ya miaka mitano watoto 82 wametelekezwa wakike 29 na kiume 53”Alieleza Meisha.
Alisema pamoja naelimu ambayo wamekuwa wakiendelea kuitoa kwa wananchi vitendo hivyo vuimekuwa vikiongezeka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mikesha ya dini inayohusisha watoto wadogo ambapo baadhi ya wanaume hutumia mikesha kuwalaghai na kuwabaka watoto wa kike.
Mkuu wa Wilaya ya Ileje Anna Gidarya amepiga marufuku mikesha ya dini hivi karibuni kwa watoto wadogo ili kuwalinda watoto dhidi yaunyanyasaji na ukatili uliokithiri wilayani humo kwa upande wa watoto wa kike.
Alitoa agizo hilo wakati wa Ziara yake ya kupokea kero za Wananchi katika vijiji vya Ishinga kata ya Ndola na Sapanda kata ya Ngulilo
Alisema mikesha mingi ya makanisa inayofanyika katika Wilaya hiyo imekuwa miongoni mwa chanzo Cha watoto wa kike kufanyiwa vitendo vya ukatili usiku hasa ubakaji na kupelekea ongezeko la mimba za utotoni.
Gidarya alisema kuwavitendo vya ukatili kwa watoto vinaongezeka wilayani humo huku mikesha ya makanisa inayohusisha watoto ikishamiri siku hadi siku hali inayopelekea baadhi yao kutumia nafasi hiyo kushawishiwa kushiriki vitendo viovu.
"Baadhi ya watu wenye nia ovu wamekuwa wakitumia mwanya huo wa mikesha kuwalaghai na kuwabaka watoto na kuwasababishia mimba za utotoni na kuharibu kabisa ndoto za maisha kwa watoto wa kike,
Tunataarifa zakutosha kuhusu watoto kufanyiwa ukatili na baadhi ya watu wakiwemo viongozi wa makanisa, naombeni kila mtu achukue jukumu la kumlinda mtoto wa kike , vitendo hivi havivumiliki kabisa" alihimiza Gidarya
Gidarya amewaagiza viongozi wa vijiji vyote na kata zote kuhakikisha, wanawachukulia hatua na kutoa taarifa za wazazi na walezi watakao kiuka na kuruhusu watoto wao kuhudhuria mikesha hiyo ya usiku.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.