Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt Dorothy Gwajima amesema kuwa Serikali inajiandaa kukamilisha uanzishaji wa baraza la wazee la Taifa ifikapo Mwaka 2022 kwa lengo la kuwawezesha wazee kujadili changamoto zinazowakabiri.
Amebainisha hayo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na mkurugenzi wa shirika la kimataifa la Kutetea na kulinda haki za wazee nchini Tanzania Helpage, Smart Daniel wakati wakijadili mikakati ya uboreshaji wa huduma za wazee hapa nchini.
Aidha Dkt Gwajima Ametoa wito kwa shirika la Helpage International kuwaandaa vijana kufanya kazi kwa ajili ya kujiwekea akiba ya baadaye ili watakapo zeeka wasitegemee misaada ya serikali na taasisi za kimataifa na madara yake wawe na uwezo wa kujimudu kimaisha.
Amesema kuwa wazee wakiandaliwa vizuri watakuwa msaada mkubwa kwa jamii inayowazunguka na Taifa kwa ujumla kuwa watakuwa wameimika vizuri katika masuala ya Elimu,kiuchumi na usitawi wa jamii ili wasiende kulelewa kwenye kambi za wazee
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya Afya inayohusisha wazee hapa nchini, mkurugenzi wa shirika la kinataifa la kutetea na kulinda haki za wazee Tanzania Helpage,Smart Daniel ameiomba serikali kuandaa sheria ya wazee ili wapate huduma bora na kupewa nafasi zinazostahili ikiwemo ishirikishwaji katika vyombo vya maamzi.
amesema Helpage Intenational limeanzisha programu maalumu ya uelimishaji jamii ikiwemo wazee wajitokeze kwa wingi katika zoezi linaloendelea hapa nchini la chanjo ya uviko 19 kwa lengo la kulinda Afya zao,ambapo mikoa ya kigoma,Mwanza,Simiyu,Njombe na Ruvuma tayari wamepatiwa elimu na kwamba baadhi ya wazee wamewezeshwa kupatiwa miradi mbalimbali ya maendeleo ili waweze kujikimu kimaisha.
Aidha Daniel ameiomba serikali kuhudhiria katika mikutano ya kimataifa inayolenga kutetea haki za wazee kwa lengo la kupata uzoefu jinsi mataifa mengine yanavyoweza kuwahudumia wazee na kuwapatia sitahimi zao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.