Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani amesema uvamizi wa vyanzo vya maji, kukata miti na kuchepusha maji kwa ajili ya matumizi ikiwemo kilimo na mifugo ni chanzo cha upungufu wa maji katika maeneo mengi nchini.
Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 50 ya Hospitali ya Kanda ya Rufaa Bugando (BMC), Rais Samia amesema anatambua miji mingi mikubwa inakabiliwa na uhaba wa maji unaosababisha mgao wa maji na upungufu wa umeme na kutaja sababu hizo.
“Kuna watu wanalima karibu na vyanzo vya maji haya yote mawili yanapelekea vyanzo vya maji kupungua. Yanapungua na hayaendi kule yanapotakiwa yaende."“Kwa maana hiyo mtiririko katika maeneo ambayo maji yanachukuliwa yanasafishwa na kupelekwa kwa matumizi ya watu yakiwa maji safi na salama unapungua kwa kiasi kikubwa,” amesema.
Ametaja sababu ya shida ya maji jijini Dar es Salaam ni kupungua kwa kina cha maji na kusababisha kuathiri mchakato wa kupeleka maji kwa wananchi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.