Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Dorothy Gwajima amezielekeza vituo vya kutolea huduma za afya nchini kutafuta mbinu mbadala ya kuweka akiba ya maji kwenye maeneo yao ili kukabiliana na hali ya upungufu wa huduma ya maji hapa nchini ili huduma kwa wagonjwa iendelee kutolewa.
Amebainisha hayo jana alipofanya ziara ya kushitukiza katika hospital ya Taifa Muhimbili baada ya malalamiko ya wananchi kukosa huduma kutokana na uhaba wa maji katika hospitali hiyo ambayo inahitani lita za maji 60,000 kwa siku.
Kufuatia hali hiyo Dkt Gwajima ameagiza uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na hospitali nyingine nchini kununua vifaa vya kuhifadhi maji zaidi ya lita 120 ili kuwe na hakiba ya maji ya siku mbili ili kuweza kukabiliana na changamoto hiyo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.