ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 22, 2021

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI MAPINGAMIZI KESI YA AKINA MBOWE.

 


Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imetupilia mbali hoja tatu zilizotolewa na upande wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi na kukipokea kitabu cha kumbukumbu ya mahabusu kama kielelezo.

Mbowe na wenzake hao, Halfan Bwire Hassan, Adamu Hassan Kasekwa na Mohamed Abdillahi Ling’wenya wanakabiliwa na kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Joachim Tiganga.

Uamuzi huo unahusu pingamizi la mawakili wa utetezi katika kesi hiyo, ambao walipinga kupokewa kwa kitabu cha kumbukumbu za mahabusu (Detantion Register – DR), cha Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam, cha mwaka 2020, kiwe kielelezo cha ushahidi upande wa mashtaka.

Upande wa mashtaka unaongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando uliiomba mahakama hiyo ikipokee kitabu hicho kuwa kielelezo cha ushahidi wake, kupitia kwa shahidi wa pili katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi, Ditektivu Koplo Ricardo Msemwa.

Hata hivyo jopo la mawakili wa utetezi linaloongozwa na Peter Kibatala lilipinga kitabu hicho kupokewa, huku wakitoa hoja tatu za pingamizi lao

Walidai kwamba hakuna amri ya mahakama ya kukiondoa mahakamani kielelezo hicho kwa kuwa kilishapokewa mahakamani katika kesi ndogo iliyohusu uhalali wa maelezo ya mshtakiwa wa pili, Adamu Kasekwa.

Soma uamuzi wa Jaji Tiganga alioutoa leo Jumatatu Novemba 22, 2021 Jaji Joachim

Jaji: Mahakama inaweza kutoa amri ya kutoa kielelezo pale ambapo shauri limefika mwisho au rufaa imefika mwisho. Mahakama katika amri yake inayohusu Disposal Order inahusu kama kielelezo kurudi kwa mwenyewe. Kielelezo kiharibiwe au kurudi Serikalini. Mahakama itasema kwamba ni kielelezo gani kiharibiwe kila mwisho mwezi.

Jaji: Na mwisho ni kwamba pale ambapo kielelezo kinatakiwa kubaribiwa, notisi itolewe siku 30 kabla kwa mshitakiwa, ofisi ya upelelezi, ofisi ya mwanasheria. Hiyo ndiyo namna ambapo kielelezo kinapswa kitolewe. Mahakama hii inakubaliana na upande wa utetezi kwamba Naibu Msajili hana mamlaka ya kutoa kielelezo. Mamlaka yake ni kusimamia pale kuendelea kinapokuwa kwenye chumba cha kielelezo.

Jaji: Kusimamia utolewaji au kuharibiwa kwa kielelezo hicho. Kwa namna hiyo basi ni kweli kwamba kielelezo hakiwezi kutolewa pasipo amri ya Mahakama. Hata hivyo, Mahakama inatakiwa ijielekeze katika sheria kesi hiyo. Mahakama inatakiwa kusema kwamba kielelezo kirudi kwa mwenyewe, au kiharibiwe, au kurudishwa Serikalini. Mahakama haina mamlaka ya kutolea amri nje ya kazi hizo ...

Jaji: Barua ilivyoandikwa kwa Naibu Msajili haikuwa imeeleza mambo hayo hapo juu. Mahakama ina maoni kwamba halikuwa muafaka kwa kutolea amri ya kuteketeza. Lakini Naibu Msajili ametajwa kwamba ana uwezo wa kutunza kielelezo, na kwamba kielelezo kinachotakiwa kwa kesi zaidi ya moja au mahakama zaidi ya  moja. Kutokana na hali hiyo basi ni wazi siyo kila wakati kwamba kila wakati kielelezo kinapokuwa kinatumika kinatakiwa kiwe na amri ya Mahakama.

Jaji: Kwamba kinaweza kutumika kwa kesi au mahakama zaidi ya moja  bila amri ya Mahakama. Kielelezo siyo lazima pawe na amri ya mahakama. Nimeona kwamba siyo lazima kielelezo hicho kuwa na amri ya Mahakamani.

Jaji: Kwa sababu hiyo natupilia mbali sababu zote tatu za mapingamizi ya kuzuia kielelezo hicho.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.