Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu imewahukumu viongozi wanane wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kulipa faini ya jumla ya shilingi milioni 350 au kifungo cha miezi mitano kwa kila kosa baada ya kuwakuta na hatia ya mashtaka 12.
Wabunge John Mnyika, Salum Mwalimu, Ester Matiko na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt Vicent Mashinji, kila mmoja anatakiwa kulipa faini ya Shilingi Milioni 30, na huku, John Heche, Peter Msigwa, Halima Mdee na Ester Bulaya wakitakiwa kila mmoja kulipa Milioni 40.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, yeye akitakiwa kulipa Shilingi Milioni 70 au kwenda jela miezi mitano.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.