Wafukuza upepo kutoka nchini Kenya wamezidi kuudhihirishia ulimwengu kuwa wao bado ni vinara wa marathon mbio ndefu mara baada ya kufanikiwa kuzitwaa medali zote za ushindi huku waking'ara kwa kishindo kwa washindani wa kumi bora katika mbio za Rock City Marathon zilizofanyika leo jijini Mwanza.
Rock city marathon hufanyika kila mwaka mkoani hapa ikizikutanisha nchi mbalimbali ulimwengu zikiwemo Uganda, Rwanda, Burundi, Kenya, Afrika ya Kusini, China na wenyeji Tanzania nazo zikizidi kuwa bora mwaka hadi mwaka.
Katika mbio hizo zilizofanyika mapema hii leo katika viwanja wa Rock Mall, mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kigwangalla.
Washiriki kutoka Kenya kila mwaka wamekuwa wakionekana ni bora zaidi, ikilinganishwa na nchi nyingine zinazoshiriki mbio za kilomita 21 na 42.
Mshindi wa kwanza wa mbio za kilomita 21 upande wa wanaume ni Bernard Musau, mshindi wa pili ni Ochieng Julius kutoka Uganda.
Mshindi wa tatu ni Alex Nizemana kutoka Rwanda, mshindi wa nne ni Willy Rono kutoka Kenya huku mshindi wa tano ni Chacha Buroyi wa Tanzania.
Kwa upande wanawake mshindi wa kwanza hadi wa nne wote ni kutoka Kenya ambao ni Ester Kakuri, Vane Nyaboke, Ronah Nyabochoa na Martha Njoroge huku mshindi wa tano ni Grace Jackson kutoka Tanzania.
Kwa upande wa washindi wa kilomita 42 upande wa wanawake mshindi wa kwanza hadi wa nne wote ni kutoka Kenya huku washindi kwa upande wa wanaume wa kwanza hadi wa tatu ni kutoka Kenya wa nne ni Hamis Athuman kutoka Tanzania.
Akizungumza katika mashindano hayo, Kigwangalla amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kufuatilia na kufanya tathimini ili kuangalia mbio za marathon zinazofanyika nchini zina mchango gani katika kukuza pato la Taifa.
Alisema katibu mkuu huyo anapaswa kuangalia mbio za marathon ikiwemo Rock city marathon, Capital Marathon, Kili marathon na Serengeti Mararhon zimetoa mchango gani katika nyanja ya maendeleo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.