ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 21, 2019

WANAKIJIJI WAMWAGIA SIFA RAIS MAGUFULI KWA KUTOA AGIZO HILI KUHUSU WAO.


Na Timothy Itembe Mara

Wananchi wa kijiji cha Nyamwaga wilayani Tarime mkoani Mara wamempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kuagiza Halmashauri ya Tarime Vijijini kuhama Nyamwaga ili kusogeza huduma karibu na wananchi.

Akiongea kwa niaba ya wenzake Mwenyekiti mstaafu ,Kirigiti Sasi alisema kuwa ndoto zake alizokuwa nazo hapo nyuma ni kuona  mji wa Nyanwaga unakuwa mji mkubwa na ndoto hizo zimetimizwa .

Mstaafu huyo aliongeza kuwa yeye binafsi aliwiwa na maendeleo ambapo katika uongozi wake alishawishi Mgodi wa kuchimba madini ya dhahabu uliopo Nyamongo ACACIA na kusaini mikataba ya kutekeleza shuguli za miradi ya  maendeleo ndani ya  kijiji hicho ikiwemo kulima barabara zinazozunguka mji wa Nyamwaga pamoja na kujenga shule ya Nyamwaga sekondari hayo wameyatekeleza kumebaki kujenga walitekeleza lakini bado kuna moja hawajatekeleza kama vile ujenzi wa Chuo cha Veta na ukamilishaji wa madarasa ya kidato cha tano na sita katika shule ya JK Nyerere.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Apoll Tindwa alitumia nafasi hiyo kuwataka watumishi wake kuhamia Nyamwaga ili kuwakaribu na wananchi wa Nyamwaga katika kutoa huduma.

"Namshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa utendaji kazi wake nasi kama halmashauri tunatekeleza agizo alilotoa tarehe saba mwezi huu la halmashauri kuhamia Nyamwaga ili kusogeza huduma karibu na wananchi nami nasema watumishi wangu ifikapo mwisho wa mwezi huu wote wawe wamehamia Nyamwaga kwa sababu mimi tayari nilishahamia na mizigo yangu lengo ni kusogeza huduma kwa jamii"alisema Tindwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.