ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 16, 2019

SIMBA VS AIGLE NOIR NGOMA DRAW.

Mchezo wa kirafiki leo uliochezwa mkoani Kigoma kati ya Simba na wageni wao Aigle Noir kutoka Burundi umekamilika kwa sare ya bila kufungana.

Mchezo huo umechezwa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika jioni ya leo umeshuhudia mlinda mlango Beno Kakolanya akiendelea kuwa imara kwa kutoruhusu bao kupenya kwenye ngome yake tena.

Huu unakuwa mchezo wa pili sawa na dakika 180 kwa Kakolanya kukaa langoni kwenye mechi za kirafiki bila kuruhusu bao baada ya ule wa kwanza mbele ya Bandari kuokoa michomo minne ya moto.

Mpaka sasa Simba imecheza michezo mitatu na imeshinda miwili na imetoa sare mchezo mmoja leo mkoani Kigoma

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.