Viongozi wa dini katika wilaya ya Arumeru wamewataka wananchi kujitokeza kuandikisha majina katika daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za vijiji na vitongoji unaotarajiwa kufanyika Tarehe 24/11/2019
Hatua ya viongozi hao wa dini kuwataka wananchi kujitokeza imekuja kufuatia hatua aliyofanya mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro kuzunguka mitaani kuhamasisha wananchi kujitokeza na kujiandikisha katika daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa vijiji na vitongoji
Wakizungumzia mwenendo wa zoezi la uandikisha linavyokwenda askofu mkuu wa makanisa ya AMEC TANZANIA Askofu Baltazar Kaaya na sheikh mkuu wa wilaya ya Arumeru Sheikh Alli issa Ibrahim mbali na kupongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya wilaya ya Arumeru katika kuwahamasisha wananchi kwenda kujiandikisha wamesema kazi hiyo siyo ya serikali peke yake na inapaswa kuungwa mkono na wadau wote wanaopenda maendeleo na amani katika wilaya ya Arumeru ambapo pia wamemuhakikisha Mkuu wa wilaya ya Arumeru kuwa watasimama na serikali katika kuhakikisha wanahamasisha waumini wao kwenda kujiandikisha .
Tazama picha na video za kikao.
*Imetolewa na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arumeru *
14/10/2019
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.