Pambano hilo la Super welterweight lililopigwa Wintrust Arena,Chicago lilikuwa ni la utangulizi kuelekea pambano kuu la uzito wa juu kati ya Oleksandr Usyk na Chazz Witherspoon.
Patrick,27, alipoteza fahamu baada ya kupata majeraha ya ubongo na hivyo kukimbizwa Hospitali huko nchini Marekani ambapo alilazwa mpaka mauti yalipomkuta.
Taarifa iliyotolewa na Promota wake Lou DiBella inasema kuwa, Patrick alifariki akiwa amezungukwa na familia yake, marafiki zake wa karibu na watu wa timu yake ya ngumi.
Wakati Patrick alipokuwa mahututi hospitali, mpinzani wake Mmarekani Charles Conwell,21, aliandika barua ya masikitiko, akisema hakutaka kitu hicho kimtokee Patrick na kueleza kuwa tukio hilo limemfanya afikirie kuachana na mchezo wa ngumi, na pambano hilo linamjia mara kwa mara kichwani kwake na kujiuliza kwa nini tukio hilo limetokea kwani hakuna anayestahili limtokee.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.